Uko hapa: NyumbaniHabariDiaspora2021 09 14Article 557458

Diasporian News of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mwinyi ateua CAG na wengine 13

Dk Mwinyi ateua CAG na wengine 13 Dk Mwinyi ateua CAG na wengine 13

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameteua viongozi 14 akiwemo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dk Othman Abbas Ali.

Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mawaziri ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said, ilieleza jana kuwa Dk Mwinyi pia amemteua Dk Juma Yakuti Juma kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi, wakati Suleiman Ali Suleiman kuwa Naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi (Sera, Ufuatiliaji na Tathmini).

Taarifa hiyo ya Zena ilieleza kuwa Dk Mwinyi pia amemteua Yussuf Ibrahim Yussuf kuwa Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Dk Mwinyi pia amemteua Saumu Khatib Haji kuwa Kamishna wa Idara ya Bajeti kwenye wizara hiyo.

Haji Ali Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sera za Kodi na Fedha, Suleiman Mohamed Rashid Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Mohamed Hassan Khamis kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti kwenye wizara hiyo.

Mwingine ni Siti Abbas Ali kuwa Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umasikini wakati Ahmed Makame Haji ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Ukuzaji Uchumi na Khamis Issa Mohammed ameteuliwa kuwa Ofisa Mdhamini Tume ya Mipango, Pemba.

Katika uteuzi huo ulioanza jana, Dk Mwinyi amemteua Dk Mohamed Juma Abdalla kuwa Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii wakati Hafsa Hassan Mbamba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Aviwa Issa Makame anakuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Maendeleo ya Utalii katika kamisheni hiyo.