Uko hapa: NyumbaniInfosDiaspora2020 09 25Article 510262

Diasporian News of Friday, 25 September 2020

Chanzo: Zanzibar 24

NITAENDELEA KUKUTANA NA WATU WA NGAZI YA CHINI HATA KWENYE UONGOZI WANGU

NITAENDELEA KUKUTANA NA WATU WA NGAZI YA CHINI HATA KWENYE UONGOZI WANGU

Mgombea wa urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema endapo atakuwa rais atahakikisha kuwa ataweka bandari na gati kwaajili ya wavuvi kwani uvuvi na utalii ndio sekta mama visiwani Zanzibar.

Hayo ameyasema leo Septemba 24 wakati akizungumza na watu wa makundi tofauti ikiwemo wavuvi, wakulima wa mwani, wafugaji wa samaki na waanika madaagaa huko katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort mazizizni nje kidogo ya mjia wa zanzibar.

Dk. Hussein emesema kupitia ziara zake tofauti alizofanya na kuwatembelea watu hao amegundua kuwa wanachangamoto nyingi zinazowakabili na kuahidi kuzitatua kwa haraka mara baaba ya kuwa rais.

Aidha Dk. Hussein amewataka wananchama wa chama cha Mapinduzi na wananchi wote kwa ujumla kuwachagua viongozi wote wa chama hicho kwanzia rais hadi diwani ili kutekeleza yale yote aliwaahidi.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi amesema kitendo cha Dk. Hussein kukutana na watu wa makundi maalum sio jambo geni kwani aliwahi kukutana na watu kama hao huko kisiwani Pemba na haitaishia kwenye kampeni tu bali taha kwenye uongozi wake.

Join our Newsletter