Uko hapa: NyumbaniHabariDiaspora2021 10 12Article 562843

Diasporian News of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kupitia maoni ya 'hadhi maalum' kwa Diaspora

Balozi Liberata Mulamula Balozi Liberata Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa Serikali ipo katika hatua ya uchambuzi wa maoni kwa ajili ya kukamiisha mchakato wa 'Hadhi Maalum' kwa watanzania waishio nje ya nhi.

Ametoa kauli hiyo akiwa katikamji wa Roma nchini Italia wakati akizungumza na Jumuiya ya Watanzania waishio nchini humo.

Amesema tayari mchakato wa awali wa kukusanya maoni kutoka kwa Wadau wote wakiwemo Diaspora umekamilika, na sasa wataalam wako katika hatua za uchambuzi wa maoni hayo.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa mchakato wa 'hadhi maalum' utakapokamilika utatoa haki za kiraia kwa Watanzania waishio nje ya nchi, isipokuwa kushiriki katika siasa kwa kuwa suala hilo linahitaji mapitio ya kikatiba.

Amewaeleza Watanzania hao wanaoishi nchini Italia kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatambua mchango unaofanywa na Diaspora katika kujitafutia maendeleo yao na kuwataka kuendelea kuwa wazalendo kwa kushiriki katika kuijenga Tanzania kwa kuitangaza vyema kibiashara na kuleta wawekezaji katika sekta mbalimbali.