Uko hapa: NyumbaniBiasharaUchumiBudgets of Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA
DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU (MB),
AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI
KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA
MWAKA 2021/22
10 Juni 2021 Dodoma

“Kwa upande wa wafanyabiashara, nawahimiza kulipa kodi stahiki
kwa Serikali. Si haki wala si uungwana kwa wafanyabiashara
kukwepa kulipa kodi. Kufanya hivyo kutaifanya Serikali yetuhindwe kutoa huduma muhimu kwa wananchi. Hospitali zetu
zitakosa dawa na kusababisha vifo, Watumishi watakosa
mishahara na haki zao Stahiki na wanafunzi watakosa elimu bure
ambayo ni zawadi tuliyowapa.”

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
14 Mei 2021

I. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu lipokee, lijadili na kukubali kupitisha Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2021/22. Hotuba hii
inawasilisha bajeti ya kwanza ya Kipindi cha Kwanza cha Serikali ya
Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mapendekezo
ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali katika Bunge lako
Tukufu yanawasilishwa kwa mujibu wa Ibara ya 137 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa
pamoja na Kifungu cha 23 (3) cha Sheria ya Bajeti, Sura 439
pamoja na Kifungu cha 124 (4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Juni 2020.

2. Mheshimiwa Spika, pamoja na hotuba hii ninawasilisha
vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina Bajeti ya Serikali. Kitabu cha
Kwanza ni Makadirio ya Mapato; Kitabu cha Pili ni Makadirio ya
Matumizi ya Kawaida kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala
wa Serikali; Kitabu cha Tatu ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida
kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
Kitabu cha Nne ni Makadirio ya Matumizi ya Maendeleo kwa Wizara,
Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, Muswada wa Sheria ya Fedha
wa mwaka 2021 pamoja na Muswada wa Sheria ya Matumizi ya
Serikali wa mwaka 2021 nayo ni sehemu ya bajeti hii.

3. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha
kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2021/22. Aidha, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kuendelea kuijalia nchi yetu amani, umoja na mshikamano na
kutupatia kiongozi mwadilifu, thabiti na imara chini ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM).

4. Mheshimiwa Spika, huu ni Mkutano wa kwanza wa Bunge
la Bajeti baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
uliofanyika Oktoba 2020, ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kilipata ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza nchi yetu. Ushindi
mkubwa na wa kishindo uliopatikana kwa CCM umedhihirisha siyo
tu imani kubwa ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi, bali pia ni
matarajio na kiu kubwa waliyonayo ya maendeleo kwa Taifa letu.

5. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa tarehe
17 Machi, 2021 Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa kuondokewa na
aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli. Naomba kutoa pole kwa Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Bunge lako Tukufu, Wanafamilia hususan Mama Janeth Magufuli na
Watanzania wote kwa msiba huo mzito. Hayati Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli ataendelea kukumbukwa kwa uongozi wake
shupavu wenye uthubutu na uzalendo wa hali ya juu ulioleta
mabadiliko chanya ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu. Mwenyezi
Mungu aipumzishe Roho yake mahali pema peponi. Amina! Aidha,
napenda kuchukua fursa hii kutoa pole kwa Watanzania kwa
kuondokewa na Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
na Mhandisi Balozi John William Herbert Kijazi, aliyekuwa Katibu
Mkuu Kiongozi. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu hao
mahali pema peponi. Amina!

6. Mheshimiwa Spika, kipekee nitumie fursa hii kumpongeza
kwa dhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa
Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi
Mkuu wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi yetu.
Mheshimiwa Spika naomba Niweke Ufunguo, Katika Hotuba
yangu popote nitakapo tumia neno “MAMA YETU” Nitakuwa
namaanisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Katika
muda mfupi wa uongozi wake, MAMA YETU ameonesha dhahiri 4
kuwa ni kiongozi makini, shupavu, mchapa kazi, mwadilifu, msikivu
na aliye na dira thabiti ya kuendelea kuiletea nchi yetu maendeleo
makubwa.

Aidha, ninampongeza “MAMA YETU” kwa kupata kura
zote za ndio za wajumbe 1,862 wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM
kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi. Wana CCM na
watanzania kwa ujumla wana imani kubwa sana kwake katika
kukiongoza Chama kwa kuzingatia misingi ya Katiba ya Chama Cha
Mapinduzi hasa ukizingatia uzoefu wake wa miaka 20 ya uongozi
ndani ya chama. Hongera sana Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi. Ninawaomba watanzania wote kila mmoja
kwa imani yake tuendelee kumuombea Mheshimiwa Rais ambaye
pia ndiye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ili Mwenyezi Mungu
aendelee kumjalia afya njema, hekima na busara katika kutekeleza
majukumu yake na “KAZI IENDELEE”.

7. Mheshimiwa Spika, hotuba hii inawasilisha Bajeti ya kwanza
ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye
Dira na Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita ya “Kudumisha
mazuri ya Awamu zilizopita, Kuyaendeleza mema yaliyopo
na Kuleta mengine mapya.

Hivyo, makadirio ya bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2021/22 yameandaliwa kwa kuzingatia nyaraka na
miongozo mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 ambao umeandaliwa kwa
kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya
CCM ya mwaka 2020 - 2025; Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki
2050; Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063; Malengo ya Maendeleo
Endelevu 2030; Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo; na
makubaliano mengine ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania
imeyaridhia.

Aidha, Bajeti imezingatia kikamilifu maeneo ya
kipaumbele yaliyoainishwa katika Hotuba ya Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati
akilihutubia Bunge hili tarehe 22 Aprili 2021.

8. Mheshimiwa Spika, naomba kurejea baadhi ya maeneo
yaliyobainishwa katika Hotuba ya Mheshimiwa Rais ambayo
yamezingatiwa katika bajeti hii kama ifuatavyo: Kudumisha Tunu za
Taifa yaani Amani, Umoja na Mshikamano ambavyo ni msingi mkuu
wa maendeleo wa Taifa letu; kuendelea kutekeleza kikamilifu
Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini kwa kufanya
marekebisho ya Sera, Sheria na kanuni mbalimbali ili kuvutia
uwekezaji wa sekta binafsi na kuongeza fursa za ajira; kufanya
maboresho ya mfumo wa utozaji na ukusanyaji wa kodi ili
kurahisisha ulipaji wa kodi na kuongeza wigo wa walipa kodi; na
kuendelea kuimarisha uendeshaji wa mashirika ya umma ili yaweze
kujiendesha kwa faida na kutoa gawio na mchango stahiki kwa
Serikali.

9. Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ni kuongeza tija ya
mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuboresha upatikanaji wa
mitaji kwa wakulima wadogo na wawekezaji kwa kushirikisha taasisi
za fedha, ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo pamoja na benki
nyingine; kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, uongezaji wa thamani
ya mazao na upatikanaji wa masoko; kukuza sekta ya viwanda
hususan vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi hapa
nchini na vyenye kuajiri watu wengi; kuendelea kuziba mianya ya
utoroshaji wa madini na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya
uchenjuaji na uchakataji wa madini nchini ili kuongeza mchango wa
sekta ya madini katika Pato la Taifa; kuimarisha miundombinu ya
usafiri, usafirishaji na nishati ikiwemo ujenzi wa barabara na
madaraja, reli, usafiri wa majini na angani, upanuzi wa bandari
pamoja na uzalishaji na usafirishaji wa umeme; kuendelea
kuimarisha na kuboresha huduma za jamii, hususan afya, elimu na
maji; na kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine, jumuiya za
kikanda na mashirika ya kimataifa.

II. TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA
2020/21

Mwenendo wa Mapato

10. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2020/21,
Serikali ilipanga kukusanya jumla ya shilingi trilioni 34.88 kutoka
katika vyanzo vyote vya ndani na nje. Hadi Aprili, 2021 shilingi
trilioni 24.53 zimekusanywa sawa na asilimia 86.1 ya lengo la kipindi
hicho. Mchanganuo ni kama ifuatavyo:

(i) Mapato yaliyokusanywa kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) yalifikia shilingi trilioni 14.54, sawa na asilimia 86.9;
(ii) Mapato yasiyo ya Kodi yalifikia shilingi trilioni 1.80, sawa na
asilimia 78.5 ya lengo;
(iii) Mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani vya Mamlaka za
Serikali za Mitaa yalifikia shilingi bilioni 607.4 sawa na asilimia
88.5 ya lengo;
(iv) Misaada na mikopo nafuu iliyopokelewa ilikuwa shilingi trilioni
1.89 sawa na asilimia 70.4 ya lengo;
(v) Mikopo ya ndani ikijumuisha mikopo ya kulipa dhamana za
Serikali zilizoiva ilifikia shilingi trilioni 3.99, sawa na asilimia
95.7 ya lengo; na
(vi) Mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara ilifikia shilingi
trilioni 1.68 sawa na asilimia 88.1 ya lengo.

11. Mheshimiwa Spika, mlipuko wa UVIKO-19 umesababisha
kutofikiwa kwa baadhi ya malengo ya makusanyo ya mapato ya
ndani hususan kwa sekta za utalii, usafiri wa anga na uingizaji wa 7
bidhaa kutoka nje. Aidha, baadhi ya mashirika na taasisi
zimeathiriwa na UVIKO-19 na hivyo kupungua kwa michango na
gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Mathalani, mapato ya
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
yameathiriwa kufuatia kuporomoka kwa shughuli za utalii
kulikosababishwa na kusambaa kwa UVIKO-19 katika nchi
zinazoleta watalii wengi nchini.

12. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha lengo la mapato ya
ndani linafikiwa, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kama ilivyoainishwa
ndani ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Kufanya
Biashara Nchini (Blueprint) kwa lengo la kuchochea ukuaji wa
uchumi. Aidha, Serikali imeendelea kusimamia na kufuatilia
utekelezaji sahihi wa sheria, kanuni na taratibu za kodi; kuboresha
mifumo ya TEHAMA ikiwemo Electronic Fiscal Device Management
System (EFDMS). Vilevile, Serikali imeendelea kufuatilia kwa karibu
utendaji wa taasisi za Serikali pamoja na kuendelea kuhamasisha
utalii wa ndani.

13. Mheshimiwa Spika, misaada na mikopo nafuu iliyopokelewa
hadi Aprili 2021 ni shilingi trilion 1.89 ikilinganishwa na shilingi
trilion 1.82 mwaka 2019/20. Pamoja na athari za mlipuko wa UVIKO
-19, misaada na mikopo nafuu iliongezeka kwa asilimia 3.84
ikilinganishwa na kiasi kilichopokelewa katika kipindi kama hicho
mwaka 2019/20. Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na
Washirika wa Maendeleo ili kuwezesha upatikanaji wa misaada na
mikopo nafuu katika kuchangia bajeti ya Serikali.

14. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikopo ya nje yenye
masharti ya kibiashara, Serikali ipo katika hatua za mwisho za
majadiliano na baadhi ya Taasisi za Fedha za Kimataifa ili
kuhakikisha kiasi kilichopangwa kukopwa kinapatikana. Vilevile,
Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma kwa lengo la kuongeza 8
ushiriki wa wawekezaji kwenye soko la ndani la fedha ili kuhakikisha
kiasi kilichopangwa kukopwa kinapatikana kwa wakati.

Mwenendo wa Matumizi

15. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi kwa mwaka
2020/21 yalikuwa shilingi trilioni 34.88 ambapo shilingi trilioni 22.10
ni matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 12.78 ni matumizi ya
maendeleo. Katika kipindi cha Julai 2020 hadi Aprili 2021, jumla ya
shilingi trilioni 24.74 zimetolewa sawa na asilimia 86.8 ya lengo. Kati
ya kiasi hicho, shilingi trilioni 17.42 zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya
kawaida ambazo zinajumuisha shilingi trilioni 6.09 kwa ajili ya
mishahara, shilingi trilioni 4.49 Matumizi Mengineyo na shilingi
trilioni 6.84 kugharamia deni la Serikali.

16. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2021, jumla ya shilingi trilioni
7.32 sawa na asilimia 74.1 ya lengo zimetolewa kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo shilingi trilioni 6.24 ni
fedha za ndani sawa na asilimia 79.7 ya lengo na shilingi trilioni
1.08 ni fedha za nje sawa na asilimia 52.8 ya lengo.
17. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa Bajeti ya Serikali
kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Aprili 2021, Serikali iliendelea kutoa
fedha kwa ajili ya kugharamia maeneo ya vipaumbele
yaliyoainishwa kwenye bajeti kama ifuatavyo:

(i) Ulipaji wa deni la Serikali kwa wakati shilingi trilioni 6.84;
(ii) Ulipaji wa mishahara ya watumishi kwa wakati shilingi trilioni
6.09;
(iii) Miradi ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme
ikiwemo mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere;
na mradi wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) shilingi trilioni 1.02;9
(iv) Ujenzi na ukarabati wa Reli ikiwemo ujenzi wa Reli kwa
Kiwango cha Kimataifa shilingi trilioni 1.49;
(v) Ujenzi wa barabara, madaraja, na viwanja vya ndege shilingi
trilioni 1.15;
(vi) Ulipaji wa madeni yaliyohakikiwa ya Watumishi, Wazabuni na
Watoa Huduma, Wakandarasi na Washauri Elekezi shilingi
bilioni 965.1;
(vii) Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, elimumsingi bila ada,
uimarishaji wa vyuo vya VETA, kukuza ujuzi kwa vijana na
ujenzi wa miundombinu ya elimu shilingi bilioni 406.6;
(viii) Ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na ujenzi
na ukarabati wa miundombinu ya afya shilingi bilioni 265.8; na
(ix) Miradi ya maji mijini na vijijini shilingi bilioni 207.5.

Tathmini ya Uhimilivu wa Deni la Serikali

18. Mheshimiwa Spika, Tathmini ya Uhimilivu wa Deni la
Serikali ilifanyika Novemba, 2020 kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo,
Dhamana na Misaada SURA 134. Tathmini hiyo ilionesha kuwa
viashiria vya deni la Serikali viko ndani ya wigo unaokubalika
kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu. Katika
Tathmini hiyo, viashiria vinaonesha kuwa: uwiano wa thamani ya
sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 27.9
ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 70; uwiano wa thamani ya sasa
ya deni la nje kwa Pato la Taifa ni asilimia 17.3 ikilinganishwa na
ukomo wa asilimia 55; na uwiano wa thamani ya sasa ya deni la nje
kwa mauzo ya nje ni asilimia 113.2 ikilinganishwa na ukomo wa
asilimia 240.10

19. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa viashiria vinavyopima
uwezo wa nchi kulipa deni, matokeo yalibainisha kuwa, uwiano wa
ulipaji wa deni la nje kwa mapato ya ndani ni asilimia 13.7
ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 23 na uwiano wa ulipaji wa
deni la nje kwa mapato yatokanayo na mauzo ya nje ni asilimia 14.0
ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 21. Kwa kuzingatia viashiria
hivyo, Tanzania ina uwezo wa kuendelea kukopa kutoka ndani na
nje ya nchi ili kugharamia miradi ya maendeleo na pia ina uwezo wa
kulipa mikopo inayoiva kwa wakati.

Mwenendo wa Sekta ya Fedha

20. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka unaoishia
Aprili 2021, viwango vya riba za mikopo ya benki kwa ujumla
vilipungua na kufikia asilimia 16.58 kutoka wastani wa asilimia
16.91 Aprili 2020. Riba za mikopo za kipindi cha mwaka mmoja
zilipungua na kufikia wastani wa asilimia 16.05 kutoka asilimia 16.37
Aprili 2020. Aidha, riba za amana ziliongezeka na kufikia asilimia
6.95 kutoka asilimia 6.69 Aprili 2020. Riba za amana za mwaka
mmoja ziliongezeka na kufikia asilimia 8.77 ikilinganishwa na
asilimia 8.01 Aprili 2020. Hali hii inafanya tofauti kati ya riba za
mkopo na amana kwa mwaka mmoja (interest rate spread)
kupungua na kufikia asilimia 7.28 kutoka asilimia 8.36 Aprili 2020.
Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa sekta ya benki ili
kuongeza kasi ya kushuka kwa viwango vya riba za mikopo.

21. Mheshimiwa Spika, sekta ya benki imeendelea kuimarika
ambapo uwiano wa mali inayoweza kubadilishwa kwa muda mfupi
kuwa fedha taslimu (Liquid Assets to Demand Liabilities) ulikuwa ni
asilimia 29.63 Machi 2021, ikiwa ni zaidi ya uwiano wa chini
unaohitajika kisheria wa asilimia 20. Uwiano wa mikopo chechefu
umepungua na kufikia asilimia 9.36 Machi 2021 ikilinganishwa na
asilimia 10.50 Machi 2020. Aidha, ukuaji wa mikopo kwa sekta
binafsi ulifikia asilimia 4.8 Aprili 2021. Ukuaji wa mikopo kwa sekta
binafsi unaenda sanjari na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga 11
kuongeza ukwasi kwenye uchumi na utekelezaji wa mpango wa
Serikali wa kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Athari za UVIKO - 19

22. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi za kukabiliana
na athari za ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO-19), Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan aliunda Kamati Maalum ya Wataalamu kuchambua athari za
ugonjwa huo na kushauri namna bora zaidi ya kukabiliana nao.

Kamati ilikamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa tarehe 17 Mei
2021 ambapo, pamoja na mambo mengine, Kamati ilibaini kuwa
Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani imeathirika kiuchumi na
kijamii kutokana na UVIKO-19 hasa katika sekta muhimu zikiwemo
afya, utalii, biashara, usafirishaji, sanaa na burudani, ambazo
zimesababisha kushuka kwa mapato yatokanayo na mauzo ya
huduma nje, akiba ya fedha za kigeni na kushuka kwa kasi ya ukuaji
wa uchumi.

Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali
kuhakikisha shughuli za uchumi zilizoathirika zinarejea katika hali ya
kawaida kama ilivyokuwa kabla ya mlipuko wa UVIKO-19.

23. Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 3 Mei 2021, Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
alizungumza na Bi. Kristalina Georgieva - Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa nia ya kuimarisha
mahusiano katika masuala ya kiuchumi na kijamii likiwemo suala la
mikakati ya kukabiliana na athari za UVIKO-19.

Kufuatia mazungumzo hayo, Wizara ya Fedha na Mipango imeanza
majadiliano na IMF ya mkopo wa dharura (Rapid Credit Facility -
RCF) wa dola za Marekani milioni 571. Mkopo huu ni wa masharti
nafuu kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii
zinazotokana na UVIKO-19.

III. SERA ZA BAJETI KWA MWAKA 2021/22

Shabaha za Uchumi Jumla

24. Mheshimiwa Spika, makadirio ya mapato na matumizi ya
Serikali kwa mwaka 2021/22, yameandaliwa kwa kuzingatia misingi
(assumptions) pamoja na shabaha mahsusi za uchumi jumla.
Malengo na shabaha za uchumi jumla ni kama ifuatavyo:

(i) Kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia
5.6 mwaka 2021 na kuendelea kukua kwa wastani wa asilimia
6.2 ifikapo mwaka 2023;
(ii) Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha
kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja kati ya wastani
wa asilimia 3.0 – 5.0 kwa mwaka 2021/22;
(iii) Mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) kufikia
asilimia 15.9 ya Pato la Taifa mwaka 2021/22;
(iv) Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.5 ya Pato la Taifa mwaka
2021/22 kutoka matarajio ya asilimia 12.9 mwaka 2020/21;
(v) Kuhakikisha kuwa nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada)
haizidi asilimia 3.0 kuendana na makubaliano ya nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(vi) Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi
mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa
kipindi kisichopungua miezi minne (4.0); na
(vii) Kuhakikisha kuwa viashiria vya ustawi wa jamii vinaimarika.13
Sera na Mikakati ya Kuongeza Mapato
25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Serikali
itaendelea kuweka vipaumbele zaidi katika ukusanyaji wa mapato
ya ndani. Masuala muhimu ya kuzingatia ni pamoja na kuimarisha
na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuendelea
kutekeleza hatua zifuatazo:
(i) Kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa
kuweka mazingira rafiki kwa mlipakodi kwa lengo la kuvutia
uwekezaji, ukuaji wa biashara ndogo na za kati ili kupanua
wigo wa kodi;
(ii) Kuendelea kutekeleza mpango wa kuboresha mazingira ya
biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuendelea
kuwianisha na kufuta au kupunguza viwango vya kodi, tozo na
ada kero;
(iii) Kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani
yakijumuisha mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa
kuhimiza matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA;
(iv) Kuendelea kuboresha Mfumo wa Serikali wa Kieletroniki wa
ukusanyaji wa mapato (GePG) na kuhakikisha taasisi zote za
Serikali zinatumia mfumo huo;
(v) Kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji katika taasisi na Mashirika ya
Umma ili kuhakikisha kuwa gawio na michango stahiki
inawasilishwa kwa wakati;
(vi) Kuimarisha usimamizi wa sheria za kodi ili kutatua
changamoto za ukwepaji kodi na kupunguza upotevu wa
mapato;
(vii) Kuhamisha jukumu la uwekaji vinasaba kwenye mafuta ya
petroli kutoka kwa mkandarasi binafsi kwenda Shirika la 14
Viwango Tanzania (TBS) ili kuhakiki ubora wa mafuta
yanayoingizwa nchini na kudhibiti ukwepaji kodi kutokana na
uchakachuaji unaofanywa kwenye mafuta yanayopita hapa
nchini; na
(viii) Kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa mikakati na miradi ya
kuongeza mapato.

26. Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizo za kuimarisha
ukusanyaji wa mapato ya ndani, Serikali itaendelea kutoa elimu
kwa umma ili kuhamasisha ushiriki wa wawekezaji kwenye soko la
ndani la fedha na kuorodhesha Hatifungani za Serikali katika Soko la
Hisa la Dar es Salaam. Aidha, Serikali itaendelea kutekeleza
masuala yaliyoainishwa katika Mwongozo wa Ushirikiano wa
Maendeleo (Development Cooperation Framework - DCF) ili
kuwezesha upatikanaji wa misaada na mikopo ya masharti nafuu na
kukopa kwa utaratibu wa udhamini kutoka taasisi za udhamini wa
mikopo (Export Credit Agencies -ECA), ambayo masharti yake yana
unafuu.

Sera za Matumizi

27. Mheshimiwa Spika, Sera za Matumizi katika mwaka
2020/21 zitajumuisha yafuatayo:

(i) Kuelekeza fedha kwenye maeneo ya kipaumbele
yatakayochochea ukuaji wa uchumi na kuhakikisha kuwa
miradi inayoendelea inapewa kipaumbele kabla ya miradi
mipya;
(ii) Kuhakikisha kuwa nakisi ya bajeti haizidi asilimia 3.0 ya Pato
la Taifa kuendana na vigezo vya Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(iii) Kudhibiti uzalishaji na ulimbikizaji wa madeni;
(iv) Kuendeleza nidhamu ya matumizi ya fedha za umma; na15
(v) Kuongeza matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Serikali ili
kuongeza ufanisi ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa
wataalamu wa ndani kwenye eneo la usalama wa mifumo
(systems security).

28. Mheshimiwa Spika, ili kuendelea kuimarisha usimamizi wa
fedha za umma kwa taasisi zinazotoza ada, Serikali inaweka
utaratibu mpya na endelevu wa kusimamia mapato na matumizi ya
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) na Wakala wa Meli Tanzania (TASAC). Hivyo,
kuanzia mwaka 2021/22, mapato yataendelea kukusanywa na
taasisi hizo kupitia mfumo wa GePG na kuingizwa kwenye akaunti
za makusanyo (holding account) zilizopo Benki Kuu. Aidha, taasisi
hizi zitapatiwa fedha kulingana na bajeti iliyoidhinishwa na fedha
kutolewa kwenye akaunti ya makusanyo baada ya kupata ridhaa ya
Mlipaji Mkuu wa Serikali. Vilevile, Serikali itafanya ufuatiliaji wa
matumizi ya taasisi hizi kila robo mwaka.

29. Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudia utaratibu wa utoaji
fedha kwa Taasisi za Uhifadhi (TANAPA, NCAA, TAWA) ili kuongeza
ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Katika kutekeleza
azma hii Serikali itatoa fedha za matumizi mengineyo kwa miezi
miwili unapoanza mwaka wa fedha na kuendelea kutoa kwa mwezi
mmoja mmoja kila mwezi. Hatua hii itaziwezesha taasisi hizi kuwa
na akiba ya fedha za kukidhi mahitaji ya mwezi unaofuata kwa
kipindi chote cha mwaka.

Maeneo ya Kipaumbele kwa Mwaka 2021/22

30. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22
ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo
wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya
“Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya
Watu”. Bajeti hii itajielekeza katika utekelezaji wa vipaumbele 16
vilivyoainishwa katika maeneo matano (5) ya Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22. Maeneo hayo ni:
Kuchochea uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa
uzalishaji viwandani na utoaji huduma ili kuongeza thamani ya
mazao ya kilimo; kukuza uwekezaji na biashara; kuchochea
maendeleo ya watu; na kuendeleza rasilimali watu.

31. Mheshimiwa Spika, ili kuwa na uchumi shindani na
shirikishi, Serikali itajielekeza katika kugharamia miradi ambayo
itajikita katika: Kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda
na kimataifa; kusimamia utulivu wa viashiria vya uchumi jumla;
kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji; kuchochea
uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje; na kuendeleza
miundombinu na huduma za reli, barabara za kufungua fursa za
kiuchumi, kuunganisha nchi jirani, kupunguza msongamano mijini
na barabara za vijijini, madaraja, usafiri wa majini na angani,
mageuzi ya TEHAMA pamoja na kutekeleza mradi wa Tanzania ya
Kidijitali, nishati, bandari na viwanja vya ndege. Eneo hili
limetengewa jumla ya shilingi trilioni 7.44 ikijumuisha shilingi trilioni
3.13 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kielelezo.

32. Mheshimiwa Spika, miradi mingine ya kielelezo
itakayotekelezwa ni: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL);
Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga ikijumuisha
ujenzi wa reli ya kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway)
kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na
Liganga; Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga
(Tanzania); Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG)
– Lindi; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji - Ruhudji MW 358; Mradi
wa Kufua Umeme wa Maji - Rumakali MW 222; Uchimbaji wa
madini ya Nickel; Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu
za Daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam)
na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya Uvuvi
(Mbegani) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Kiwanda cha Sukari
Mkulazi; Utafutaji wa mafuta katika vitalu vya Eyasi Wembere na 17
Mnazi Bay North; Mradi wa Magadi Soda – Engaruka; Kuongeza
Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuzi wa Kati na
Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Ustawi wa Jamii; na
kuendeleza Kanda Maalumu za Kiuchumi.

33. Mheshimiwa Spika, katika eneo la kuimarisha uwezo wa
uzalishaji viwandani na utoaji huduma, msukumo utawekwa kwenye
miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya
kilimo, mifugo na uvuvi. Katika eneo hili, kipaumbele ni pamoja na:
Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji na uhifadhi wa
mazao ya kilimo; kuimarisha vituo vya utafiti na huduma za ugani;
kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi;
kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi;
kuboresha huduma za uhimilishaji mifugo; na kujenga machinjio ya
kisasa na minada ya mifugo.

34. Mheshimiwa Spika, Serikali itaweka mkazo kwenye ujenzi
wa viwanda vya kuongeza thamani ya madini pamoja na kuzalisha
bidhaa zitakazotumia malighafi na rasilimali zinazopatikana nchini.
Aidha, Bajeti hii itajielekeza katika kugharamia miradi na programu
inayolenga kuboresha huduma za utalii, fedha na bima pamoja na
kuendeleza viwanda vya uzalishaji wa dawa muhimu na vifaa tiba.
Jumla ya shilingi trilioni 1.38 zimetengwa kugharamia utekelezaji wa
miradi katika eneo hili.

35. Mheshimiwa Spika, katika eneo la kukuza uwekezaji na
biashara, Serikali itagharamia programu zitakazoimarisha masoko ya
ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa katika
kukuza biashara. Masoko yanayolengwa ni yale yatakayotoa fursa
kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, ikiwemo bidhaa zitokanazo na
mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu. Vilevile, Serikali
itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji
ikiwemo kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Biashara na
Uwekezaji (Blueprint). Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi bilioni
31.6.18

36. Mheshimiwa Spika, ili kuchochea maendeleo ya watu,
miradi itakayotekelezwa italenga kuboresha maisha ya watu kwa
kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo elimu na
mafunzo kwa ujumla, afya na ustawi wa jamii, huduma za maji na
usafi wa mazingira na kinga ya jamii ikijumuisha Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF. Aidha, Serikali itaendelea
kupanga, kupima na kumilikisha ardhi mijini na vijijini, kusimamia
na kuendeleza rasilimali za maji; na kuendelea na utekelezaji wa
programu za kulinda mazingira na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Jumla ya shilingi trilioni 4.43 zimetengwa.

37. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuendeleza rasilimali
watu, Serikali itagharamia programu inayolenga kuendeleza maarifa
na ujuzi wa rasimali watu katika ngazi zote za elimu ikiwemo
kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri. Aidha, Serikali
itaendelea kuboresha viwango vya utoaji wa elimu ya ufundi na
mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ujuzi adimu kwa lengo la
kuongeza tija na ushindani wa wananchi katika kutumia rasimali
zilizopo nchini ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Jumla ya shilingi bilioni 50.5 zimetengwa.

38. Mheshimiwa Spika, hotuba yangu niliyowasilisha leo
asubuhi ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango
wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 imeainisha kwa kina
maeneo ya kipaumbele ambayo Serikali itayatekeleza kupitia Bajeti
ya mwaka 2021/22.

39. Mheshimiwa Spika, pamoja na miradi ya kielelezo, Serikali
itatekeleza miradi mingine ya uboreshaji wa miundombinu ambayo
itagharamiwa na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki ya
Dunia. Miradi hiyo ni Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam
Awamu ya Pili (DMDP II) wa kukabiliana na mafuriko kwenye Bonde
la Mto Msimbazi utakaogharimu dola za Marekani milioni 120. Mradi
huu utahusisha ujenzi wa daraja katika eneo la Jangwani, na 19
upanuzi na ujenzi wa kingo za mto Msimbazi. Mradi wa pili
unahusisha uboreshaji wa barabara za kukuza fursa shirikishi za
kijamii na kiuchumi ambapo Benki ya Dunia itatoa dola za Marekani
milioni 300 na mchango wa Serikali ni dola za Marekani milioni 50.
Mradi huu unalenga kuboresha barabara za vijijini katika maeneo
yenye tija kubwa ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.

40. Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Serikali imeanza
mazungumzo na Benki ya Dunia kupitia dirisha la International
Development Association (IDA) kwa ajili ya mradi wa uboreshaji
miundombinu katika Majiji na Miji 45. Utekelezaji wa mradi huu
utaanza katika mzunguko wa 20 (IDA 20) unaotegemewa kuanza
Julai 2022 na utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 500.
Mradi utahusisha ujenzi wa miundombinu ya msingi ili kuboresha
mazingira ya biashara na uwekezaji kwa lengo la kukuza uchumi wa
miji husika.

Maeneo Mengine Muhimu

Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022

41. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inajiandaa kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka
2022 kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351. Kama
mojawapo ya maandalizi ya utekelezaji wa Sensa ya Mwaka 2022
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa upande wa Tanzania Bara na Ofisi ya
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar imekamilisha kuandaa Kitabu
cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa ya Watu na
Makazi ya Mwaka, 2022. Kitabu hiki kinaainisha namna ya usimamizi
na utekelezaji wa zoezi zima la Sensa, gharama ya kufanya Sensa
pamoja na muundo wa Sensa utakavyokuwa katika ngazi zote za
kiutawala.

42. Mheshimiwa Spika, jumla ya shilingi bilioni 328.2
zinatarajiwa kutumika kugharamia sensa ya mwaka 2022. Kwa mara 20
ya kwanza katika historia ya Sensa nchini, Sensa ya Mwaka 2022
itatumia teknolojia ya vishikwambi (tablets) katika utengaji wa
maeneo ya kijiografia na ukusanyaji wa takwimu uwandani.
Matumizi ya teknolojia hii yana manufaa makubwa, hasa katika
kupunguza gharama na muda wa kukusanya na kuchakata takwimu,
hali inayowezesha kutoa matokeo ya Sensa ndani ya muda mfupi.

43. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa zoezi la Sensa ya Watu na
Makazi ni jukumu la kila mtu, natoa wito kwa kamati zote za Sensa,
Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote, Waheshimiwa Wabunge pamoja
na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa
kutosha katika maandalizi ya Sensa na wajitokeze wote siku ya
kuhesabu watu. Lengo ni kuhakikisha Watu waliolala nchini usiku
wa kuamkia siku ya Sensa (usiku wa sensa) wanahesabiwa na
kuchukuliwa taarifa zao za kiuchumi, kijamii, mazingira na makazi
wanayoishi na mengine mengi kwa ajili ya kupanga mipango
endelevu ya maendeleo ya wananchi.

Maslahi ya Wafanyakazi

44. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua na kuthamini
mchango wa watumishi wa umma na wa sekta binafsi katika kukuza
Pato la Taifa. Kwa kutambua hilo, Serikali itachukua hatua
mbalimbali za kuboresha maslahi ya wafanyakazi kama ifuatavyo:

(i) Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya
ajira (PAYE) kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8. Hatua hii ni
mwendelezo wa juhudi za Serikali za kupunguza mzigo wa
kodi kwa wafanyakazi, ambapo kiwango hicho kimepunguzwa
kutoka asilimia 11 mwaka 2015/16 hadi asilimia 8 itakayoanza
kutekezwa mwaka 2021/22;
(ii) Kufuta tozo ya asilimia 6 iliyokuwa ikitozwa kwa ajili ya
kulinda thamani ya mkopo wa elimu ya juu (Value Retention
Fee) kwa wanufaika; na21
(iii) Kutenga jumla ya shilingi bilioni 449 kwa ajili ya kuwapandisha
vyeo watumishi 92,619.
Maslahi ya Madiwani, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata

45. Mheshimiwa Spika, Madiwani wenzetu wanafanya kazi nzuri
sana za kusimamia shughuli za maendeleo kwenye kata zetu. Hawa
ni wabunge wakaazi wa kwenye kata zetu ambao kila siku wako na
wananchi wetu kwenye kusimamia shughuli za maendeleo. Hata
hivyo, katika baadhi ya halmashauri madiwani wamekuwa
wakikopwa posho zao, na wengine hufikia hatua ya kupiga magoti
kwa wakurugenzi watendaji ili walipwe. Hali hii imekuwa ikipunguza
ufanisi katika halmashauri zetu kwa madiwani wengi kufanya
maamuzi yanayopendekezwa na wakurugenzi watendaji hata kama
hayana maslahi kwa Taifa ili waweze kulipwa posho zao. Jambo hili
limeongelewa kwa hisia kali sana na Waheshimiwa Wabunge hapa
bungeni.

Waheshimiwa Wabunge na Waheshimiwa Madiwani,
napenda niwaeleze kuwa MAMA YETU amesikia kilio chenu na
alinielekeza mimi pamoja na Waziri wa TAMISEMI kulitafutia
ufumbuzi suala hili.

46. Mheshimiwa Spika, napendekeza kuanzia mwaka 2021/22,
Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za Waheshimiwa
Madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa
Halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato. Halmashauri 16
zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A) zitaendelea kutumia
mapato yake ya ndani kulipa posho za Madiwani kupitia kwenye
akaunti zao.

47. Mheshimiwa Spika, Maafisa Tarafa ni viunganishi muhimu
wa ngazi za kata na Wilaya zetu ambapo wengi wao hufanya kazi
nzuri sana ya kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya Serikali katika
maeneo yao. Kwa kutambua umuhimu wao, Serikali ya CCM
iliwapatia pikipiki viongozi hawa ili waweze kufanya kazi zao vizuri. 22
Hata hivyo, wengi wao wanashindwa kugharamia ununuzi wa
mafuta na matengenezo ya vitendea kazi hivi na kulazimika
kuwachangisha wananchi na hata wengine kuomba msaada kwa
wadau mbalimbali. Hali hii inapunguza sana ufanisi katika Tarafa
zetu. Kupitia hotuba hii, napenda niwajulishe Maafisa Tarafa wote
nchini kuwa MAMA YETU amesikia kilio chenu. Hivyo, napendekeza
kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho ya shilingi
100,000/= kwa mwezi kwa kila Afisa Tarafa ili waweze kumudu
gharama za mafuta na matengenezo ya pikipiki.

48. Mheshimiwa Spika, Watendaji Kata ndio wasimamizi wa
kazi za sekta zote na ni watendaji wakuu kwenye kata. Wengi wao
wanafanya kazi katika mazingira magumu ili kufanikisha shughuli za
maendeleo katika kata zetu ikiwemo kusimamia ukusanyaji wa
mapato na masuala ya usalama. Idadi kubwa ya watendaji hawa
hutumia mishahara yao kufanya kazi mbalimbali ikiwemo ufutiliaji
wa mapato ya Serikali kwa kukodi pikipiki ili kufanikisha shughuli
zilizopo.

Kwa ujumla wanafanya kazi nzuri sana ya kusimamia
shughuli za maendeleo kwenye kata zetu. Jambo hili limeongelewa
kwa hisia kali sana na Mheshimiwa Rose Busiga, Mbunge wa Viti
Maalum (Geita), ambaye ni mtendaji wa kata mstaafu na kuungwa
mkono na wabunge wengi hapa bungeni. Waheshimiwa wabunge,
MAMA YETU amesikia kilio hiki na kutuelekeza kulitafutia ufumbuzi
suala hili. Hivyo, napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali
kuanza kulipa posho ya shilingi 100,000/= kwa mwezi kwa kila
Mtendaji Kata kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokuwa
yakitumika kulipa madiwani.

Madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

49. Mheshimiwa Spika, wastaafu wetu walilitumikia Taifa hili
kwa uzalendo, uadilifu na bidii kubwa sana. Hatuwezi kuhesabu
mafanikio ya nchi yetu bila kutaja mchango wa wazee hawa.
Kumekuwepo na changamoto za muda mrefu za ulipaji wa mafao
yao kutokana na ufanisi mdogo wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika
kuhudumia wastaafu wetu. Hali hiyo kwenye mifuko yetu23
imechangiwa, pamoja na mambo mengine, na uwepo wa madeni
ambayo mifuko inaidai Serikali na hivyo kusababisha wastaafu wetu
kukosa au kusubiri kwa muda mrefu ili kulipwa mafao yao. Jambo
hili pia limejadiliwa kwa hisia kali na Waheshimiwa Wabunge hapa
bungeni.

Wazee wetu hawa hupata shida sana, ambapo baadhi yao
hufadhiliwa malazi kwa kulala misikitini na makanisani na wengine
hutegemea wahisani kuhudumia familia zao kinyume na mchango
walioutoa katika ujenzi wa nchi hii. MAMA YETU amesikia kilio cha
wazee hawa na kutuelekeza Wizara ya Fedha na Mipango
kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kukamilisha zoezi la kitaalamu
ili kujua hali halisi ya madeni na namna bora ya kulipa madeni hayo.

50. Mheshimiwa Spika, napendekeza kulipa madeni
yanayodaiwa na mifuko kwa kutenga fedha kwenye bajeti na
kutumia utaratibu wa kutoa hatifungani maalum isiyo taslimu (Noncash Special Bond) zitakazoiva kwa nyakati tofauti kuanzia miaka
miwili hadi 25. Utaratibu wa hatifungani una faida mbalimbali
zikiwemo: kuipa Serikali nafasi ya kibajeti ya kuendelea kutekeleza
miradi mingine ya maendeleo; kuiwezesha Serikali kuyatambua
madeni hayo kwenye kanzidata ya madeni; na kuzuia madeni hayo
kuendelea kuongezeka kulingana na tathmini ya thamani ya madai
(actuarial valuation).

Aidha, utaratibu huo utaboresha mizania ya
hesabu na mtiririko wa mapato yanayotokana na riba ya hatifungani
hizo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hatua hii inakwenda kumaliza
kabisa tatizo hilo la wazee wetu kudai haki yao kwa damu na
machozi yaliyodumu kwa muda mrefu.

51. Mheshimiwa Spika, Serikali imepokea malalamiko kuhusu
kucheleweshwa kwa michango ya watumishi kupelekwa kwenye
mifuko ya hifadhi ya jamii na baadhi ya ofisi za Serikali kutopeleka
kabisa michango hiyo. Jambo hili limekuwa likisababisha usumbufu
kwa watumishi punde wanapostaafu. Hivyo, napendekeza kulipa
michango hiyo moja kwa moja kutokea Hazina kwa taasisi zote
ambazo watumishi wanalipwa na Hazina. Taasisi ambazo zinalipa
watumishi kutokana na vyanzo vyao vya mapato zitaendelea 24
kupeleka michango ya watumishi wao kwa ufuatiliaji wa karibu wa
Serikali. Serikali itafanya uhakiki na kulipa madeni ya michango
ambayo haijawasilishwa kwenye mifuko hadi sasa.

Jeshi la Polisi

52. Mheshimiwa Spika, katika jeshi la polisi kwa askari
wapiganaji, kuna utaratibu wa wapiganaji kufanya kazi kwa
mikataba ya muda mfupi kwa miaka 12 kabla hawajapata ajira za
kudumu. Jambo hili huwasababishia wapatapo mkataba wa kudumu
wawe wamechelewa kwa miaka 12 ikilinganishwa na mtumishi
mwingine aliyeingia pamoja kazini katika idara nyingine. Jambo hili
linamadhara hasi katika itifaki ya utumishi na mafao ya mpiganaji
anapostaafu. Hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu cha askari wa
Jeshi la Polisi. Kutokana na changamoto hiyo, MAMA YETU amesikia
kilio cha askari hao na alituelekeza tukae na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi ili kutafuta suluhisho la jambo hili.

Napendekeza
kuanzia mwaka 2021/22 askari wa Jeshi la Polisi wataingia mkataba
wa kipindi cha miaka 6 na kuingia katika ajira ya kudumu.

Kurahisisha Kasi ya Utekelezaji wa Miradi

53. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi na ufanisi
katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango
itafanya mabadiliko katika Kanuni ya 21 ya Sheria ya Bajeti, SURA
439 ili kuondoa changamoto iliyopo ya fedha ambazo hazijatumika
hadi tarehe 30 Juni kila mwaka kurejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina
ya Serikali. Mabadiliko hayo yatatoa fursa kwa Maafisa Masuuli
kuwasilisha taarifa ya fedha kuvuka mwaka hadi tarehe 30 Juni
kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali badala ya siku 15 kabla ya mwaka wa
fedha kumalizika. Fedha hizo zitawekwa kwenye Akaunti ya Amana
kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli ambazo hazijakamilika wakati
wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha husika. Kwa
msingi huo, kuanzia sasa hakutakuwa na fedha zenye miadi
zitakazorejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ifikapo tarehe 25
30 Juni ya kila mwaka wa fedha isipokuwa pale ambapo Maafisa
Masuuli wamekiuka masharti ya Sheria ya Bajeti, SURA 439 na
Sheria ya Fedha za Umma, SURA 348.

Kodi ya Majengo

54. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na changamoto kubwa katika
ukusanyaji wa kodi ya majengo, hali iliyosababisha Serikali kubadili
njia za ukusanyaji mara kwa mara. Kabla ya mwaka 2017/18,
Serikali za Mitaa zilikuwa na jukumu la kukusanya mapato hayo
lakini hazikufanya vizuri. Kuanzia mwaka 2017/18, Serikali ilitumia
Mamlaka ya Mapato kukusanya kodi hiyo, ambapo pia haikufanya
vizuri. Ukusanyaji wa kodi hii kwa kutumia Serikali za Mitaa au TRA
umekuwa ukitumia njia za kizamani ambazo zinahusisha watu
kusafiri, kupanga foleni na kukusanya fedha taslimu (cash).

Utaratibu huu unatumia gharama kubwa, muda na ni hatarishi kwa
mapato. Katika kuhakikisha kodi hii inafikia malengo, Serikali
imeandaa utaratibu mzuri wa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa
kodi ya majengo.

Kodi ya Wajasiliamali

55. Mheshimiwa Spika, wafanyabiashara na watoa huduma
wadogo nchini wameendelea kutambulika kupitia vitambulisho vya
wajasiriamali. Tangu kuanza kwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya
wafanyabiashara na watoa huduma wadogo nchini, jumla ya
vitambulisho 2,335,711 vimegawiwa ambavyo vimewezesha
kukusanya jumla ya shilingi bilioni 46.71. Lengo ni kuendelea
kuwatambua wafanyabiashara wadogo na kuwawekea mazingira
rafiki ya ufanyaji biashara. Katika mwaka 2020/21, Serikali imefanya
maboresho ya vitambulisho hivyo kwa kuweka picha na jina la
mjasiriamali ili kuongeza udhibiti na kufungua fursa kwa
wajasiriamali kuweza kutumia vitambulisho hivyo kupata huduma za
kibenki na bima ya afya.

Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea na
uratibu wa kugawa vitambulisho hivi kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Mapato Tanzania ambayo ndiyo yenye mfumo wa kusajili 26
wafanyabiashara hao, kuchapisha vitambulisho na kuwapatia
Halmashauri husika kwa ajili ya kugawa.

IV. MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA NA TOZO
MBALIMBALI

56. Mheshimiwa Spika, napenda sasa kuwasilisha mbele ya
Bunge lako Tukufu mapendekezo ya kufanya marekebisho ya
mfumo wa kodi, ikiwemo baadhi ya viwango vya kodi, tozo na
ada zinazotozwa chini ya Sheria mbalimbali na kurekebisha
taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya
Serikali.

Marekebisho haya yamezingatia dhamira ya Serikali ya
kurejesha ukuaji wa uchumi katika hali ya kawaida baada ya athari
zilizotokana na UVIKO-19 sambamba na kuendelea kuwa na mfumo
wa kodi ambao ni tulivu na wa kutabirika ili kuvutia uwekezaji
kutoka ndani na nje. Vile vile, marekebisho yanalenga kuchochea
kasi ya ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya kilimo na
viwanda, kuongeza kipato kwa waajiriwa na kuongeza
mapato ya Serikali.

Aidha, Serikali inaendelea kutekeleza Mpango
wa Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara (BluePrint) kwa
kuwianisha tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wizara na
Mamlaka za Udhibiti kwa lengo la kupunguza na kurahisisha ulipaji
wake au kuzifuta baadhi ya tozo na ada hizi. Marekebisho
yanayopendekezwa yanahusu Sheria zifuatazo:

(a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148;
(b) Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;
(c) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
(d) Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2004;
(e) Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438;27
(f) Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290;
(g) Sheria ya Kodi ya Majengo, SURA 289;
(h) Sheria ya Ardhi, SURA 113;
(i) Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189;
(j) Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82;
(k) Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, SURA 41;
(l) Sheria ya Ukaguzi wa Umma, SURA 418;
(m) Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, SURA 134
(n) Sheria ya Usajili wa Magari, SURA 124;
(o) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168;
(p) Sheria ya Raia wa Kigeni (Uratibu wa Ajira) Na. 1 ya mwaka
2015;
(q) Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali zinazotozwa na
Wizara, Mikoa Wakala, Mamlaka za Udhibiti na Idara
zinazojitegemea;
(r) Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria za Kodi
na Sheria nyingine mbalimbali;
(s) Kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira
ya Kufanya Biashara (Blueprint) kwa kurekebisha Ada na Tozo
mbalimbali;
(t) Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, SURA 220;
(u) Sheria ya Petroli, SURA 392; na
(v) Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306.28
A. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148

57. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 kama
ifuatavyo:

(i) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vyumba vya
ubaridi (cold rooms) vinavyotambuliwa kwa H.S Code
9406.10.10 na 9406.9010. Lengo la msamaha huu ni
kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mbogamboga na maua
nchini ili kuchochea kilimo cha kisasa;
(ii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye madini
(precious metals) na makinikia yatakayoingizwa nchini kwa ajili
ya kuchenjuliwa, kuongezewa thamani na kuuzwa kwenye
masoko ya madini yanayotambulika nchini. Lengo la pendekezo
hili ni kuviwezesha viwanda vya uchenjuaji vilivyoanzishwa
nchini kupata malighafi ya kutosha kwa ajili ya uchakataji na
hatimaye kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
(iii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma za
bima ya mifugo. Lengo la marekebisho haya ni kuchochea
shughuli za ufugaji nchini;
(iv) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa na
huduma zitakazoingizwa au kununuliwa hapa nchini kwa ajili ya
kutekeleza mradi wa mafuta ghafi (EACOP). Lengo la
marekebisho haya ni kutoa unafuu wa kodi katika utekelezaji
wa miradi tajwa;
(v) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mafuta ghafi
yanayotambulika kwa H.S Code 2709.00.00 kwa lengo la kutoa
unafuu kwa mlaji ikiwemo Kampuni ya uendeshaji wa bomba la
mafuta (EACOP);29
(vi) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye Nyasi Bandia
zinazotambulika kwa HS Code 5703.30.00 na 5703.20.00 kwa
ajili ya Viwanja vya Mpira vilivyoko kwenye Majiji. Msamaha
huo utahusisha ridhaa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania. Lengo la hatua hii ni kuendeleza michezo na kukuza
vipaji nchini;
(vii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye kadi za
kutengeneza vitambulisho vya taifa zinazotambulika kwa H.S
Code 3921.11.90.00 na malighafi nyingine za kutengeneza kadi
hizo zinazotambulika kwa H.S Code 3921.11.90.00
zitakazoingizwa nchini na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA). Lengo la pendekezo hili ni kupunguza gharama za
kutengeneza Vitambulisho vya Taifa na kuharakisha upatikanaji
wake;
(viii)Kumekwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za misaada
kwenye miradi ya maendeleo kwa hitaji la kisheria la kusubiri
idhini ya Baraza la Mawaziri likae ili kuidhinisha misamaha.
Napendekeza Kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s), kwenye
bidhaa na huduma zitakazotumika kwenye miradi
inayotekelezwa na taasisi husika. Aidha, taasisi zitakazonufaika
na msamaha huo ni zile ambazo zina mikataba na Serikali
yenye kipengele kinachotoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la
Thamani;
(ix) Sekta ya mawasiliano imekuwa ikikua vizuri na kuwa kiungo
muhimu cha kuongeza wigo wa wananchi ambao wako kwenye
ulimwengu wa kidijitali na kwenye sekta ya fedha (Financial
Inclusion). Napendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye simu janja za mkononi (smart phones) HS
Code 8517.12.00, vishikwambi (Tablets) HS Code 8471.30.00
au 8517.12.00 na modemu (modems) HS Code 8517.62.00 au
8517.69.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya 30
huduma za mawasiliano ili kufikia lengo la asilimia 80 ya
watumiaji wa intaneti ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46
iliyopo sasa;
(x) Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye
mikebe inayotumika kuhifadhia maziwa inayotambuliwa kwa
H.S Code 7310.29.20 ambayo kwa sasa haitumiki kwa ajili ya
kazi hiyo na badala yake napendekeza kutoa msamaha wa kodi
ya Ongezeko la Thamani kwenye mikebe ya kubebea maziwa
inayotambulika kwa H.S Code 7310.29.90, 7310.10.00 na
7612.90.90. Lengo la Pendekezo hili ni kuwapunguzia gharama
wazalishaji na kuchochea ukuaji wa sekta ya maziwa nchini;
(xi) Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye taa
zinazotumia umeme wa jua zinazotambulika kwa H.S. Code
85.13 na 94.05. Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha
msamaha huu sambamba na msamaha unaotolewa chini ya
Sheria ya Ushuru wa Forodha ambayo inasamehe Kodi kwenye
vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme wa jua pekee
na kurahisisha usimamizi wake. Aidha, pendekezo hili linalenga
kuweka usawa katika ulipaji kodi kwa watumiaji wa taa
zinazotumia nishati za aina zote;
(xii) Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia
sifuri kwenye huduma ya usafirishaji na huduma zinazohusiana
na usafirishaji wa mafuta ghafi kupitia bomba linalojengwa kwa
pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na Uganda (EACOP).
Lengo la pendekezo hili ni kuwezesha huduma tajwa
kutekelezwa bila kodi sanjari na uzoefu wa kimataifa kwa
bidhaa zilizopita hapa kwenda nchi jirani au ng’ambo;
(xiii) Kuzitambua bidhaa za mtaji zilizomo kwenye Sura ya 84, 85 na
90 ya Kitabu cha Ushuru wa Pamoja wa Forodha wa Afrika
Mashariki kuwa bidhaa za mtaji zitakazostahili kupata kivutio
cha ahirisho la malipo ya VAT. Lengo la pendekezo hili ni 31
kuwianisha maana ya bidhaa za mtaji kwenye Sheria za kodi na
kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali kwenye
kifungu tajwa;
(xiv) Kubadilisha utaratibu wa kutoa msamaha kwenye miradi ya
Serikali inayogharamiwa na fedha za serikali na fedha za
wafadhili ambapo mnufaika wa msamaha huo atawasilisha
maombi kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
badala ya utaratibu wa kuwasilisha kwa Waziri wa Fedha kwa
ajili ya kupata ridhaa na kutoa Tangazo la Serikali (GN) kwa
kila mradi. Utaratibu huu utarahisisha na kuharakisha utoaji wa
misamaha badala ya utaratibu wa sasa kutokana na TRA kuwa
na ofisi kwa kila mkoa nchini kote ambazo zinaweza kupokea,
kuchambua na kusimamia matumizi sahihi ya misamaha; na
(xv) Kuhusu Zanzibar, napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria
ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kurudisha utaratibu wa
kurejesha VAT kwa bidhaa zinazonunuliwa Tanzania Bara na
kutumika Tanzania Zanzibar. Hii inatokana na mfumo wa
kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwa bidhaa za
viwandani pekee kutowanufaisha wafanyabiashara wa Zanzibar
wanaonunua bidhaa na kutozwa VAT Tanzania Bara na
kutozwa tena VAT bidhaa hizo zinapopelekwa Zanzibar. Aidha,
inapendekezwa marejesho ya VAT yatakayofanyika kwa bidhaa
zinazotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar yafanyike pia kwa
bidhaa zitakazotoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara
sambamba na marekebisho ya vifungu husika vya Sheria za
VAT kwa pande zote mbili za muungano. Ili kuwa na ufanisi wa
marejesho, maboresho ya mifumo yatafanyika ili isomane baina
ya Tanzania Bara na Zanzibar. Kutokana na utaratibu huu,
kiwango cha asilimia sifuri ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
kilichokuwa kinatozwa bidhaa hizo kitasitishwa.
Hatua zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla
zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 55,499.97.32
B. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332

58. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo:
(i) Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza Kodi ya Mapato
yanayohusiana na ajira kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8 kama
ilivyobainishwa katika Jedwali Na. 1A na 1B.
Jumla ya M apato Kiwango cha Kodi
Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi
3,240,000/=
Hakuna kodi
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
3,240,000/= lakini hayazidi
shilingi.6,240,000/=
9% ya kiasi kinachozidi shilingi
3,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
12,000,000/=
Shilingi 1,566,000/= jumlisha 30% ya
kiasi kinachozidi shilingi
12,000,000/=
Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi
3,240,000/=
Hakuna kodi
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
3,240,000/= lakini hayazidi shilingi
6,240,000/=
8% ya kiasi kinachozidi shilingi
3,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
12,000,000/=
Shilingi.1,536,000/= plus 30% ya
kiasi kinachozidi shilingi
12,000,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
6,240,000/= lakini hayazidi shilingi
9,120,000/=
Shilingi 240,000/= jumlisha 20% ya
kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
9,120,000/= lakini hayazidi shilingi
12,000,000/=
Shilingi 816,000/= plus 25% ya kiasi
kinachozidi shilingi 9,120,000/=
Jedwali Na. 1A: Viwango vya sasa
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
6,240,000/= lakini hayazidi shilingi
9,120,000/=
Shilingi 270,000/= jumlisha 20% ya
kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/=
Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi
9,120,000/= lakini hayazidi shilingi
12,000,000/=
Shilingi 846,000/= jumlisha 25% ya
kiasi kinachozidi shilingi 9,120,000/=
Jedwali Na. 1B Viwango vinavyopendezwa33
Hatua hii inachukuliwa ikiwa ni dhamira ya Serikali ya muda
mrefu kuwapunguzia mzigo wa Kodi wafanyakazi. Hatua hii
inatarajiwa kupunguza mapato kwa shilingi milioni
14,178.06;
(ii) Kutoa msamaha wa Kodi ya Mapato kwenye hatifungani za
Serikali. Sheria ya Kodi ya Mapato ilisamehe Kodi ya Mapato
kwenye hatifungani kwa mwaka 2002/03 pekee. Lengo la
hatua hii ni kuhakikisha soko la ndani la hatifungani linaendelea
kusaidia kugharamia miradi ya Serikali;
(iii) Kumekuwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za kutoka
kwa nchi wahisani zinazokwenda kutekeleza Miradi ya
maendeleo. Napendekeza Kurejesha utaratibu wa Mamlaka ya
Waziri mwenye dhamana ya Fedha kutoa msamaha kwa kutoa
tangazo la Serikali (GN) bila sharti la kupata ridhaa ya Baraza
la Mawaziri kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za wafadhili
kupitia mikataba iliyoingiwa baina ya nchi hizo na Serikali
yenye kifungu kinachoruhusu msamaha wa kodi ya mapato.
Lengo la marekebisho haya ni kuharakisha utekelezaji wa
miradi inayofadhiliwa kwa misaada na mikopo yenye gharama
nafuu ambayo utekelezaji wake umekuwa ukichelewa kusubiri
ridhaa ya Baraza la Mawaziri;
(iv) Kutoza Kodi ya Zuio kwa kiwango cha asilimia mbili (2) kwenye
malipo yanayohusisha mauzo ya mazao ya kilimo, mifugo na
uvuvi yanapouzwa kwenye kampuni na mashirika yote
yanayojihusisha na usindikaji na ununuzi wa mazao. Kwa sasa,
Taasisi za Serikali pekee kama vile (Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya Chakula (NFRA) ndizo zinakata kodi hiyo kwa kiwango cha
asilimia mbili (2). Aidha, pendekezo hili halitahusisha wakulima
wadogo na wale wanaouza mazao yao kwenye masoko ya
msingi (AMCOS) na kwenye magulio. Lengo la pendekezo hili ni
kuweka usawa katika utozaji wa kodi kwa Kampuni zote
zinazojishughulisha na mazao ya Kilimo, mifugo na uvuvi.34
Pendekezo hili linatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa
kiasi cha shilingi milioni 43,954.2;
(v) Kufanya maboresho ya Sheria ya Kodi ya Mapato ili kuwezesha
ukokotoaji wa gharama za uchakavu kwa kiwango maalum cha
asimilia tano (5) kwenye gharama za mali za ujenzi wa bomba
la mafuta (EACOP). Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha
gharama za uchakavu na muda wa matumizi wa bomba husika
kwa kuzingatia masharti ya mkataba uliosainiwa baina ya
Serikali za Uganda na Tanzania;
(vi) Kuweka utaratibu maalum wa utozaji kodi kwa wachimbaji
wadogo wa madini wenye mauzo ghafi yasiyozidi shilingi
milioni 100 kwa mwaka kama ifuatavyo: -
(a) Kutoza kodi wachimbaji wadogo wa madini kwa kiwango
mfuto cha asilimia 3 kwenye thamani ya mauzo ya madini
pindi yanapopatikana;
(b) Kuweka muda wa ulipaji kodi kuwa ni wakati wanapouza
madini na kulipa mrabaha kwenye Tume ya Madini au
maeneo maalum yaliyoanzishwa chini ya sheria ya madini;
(c) Kuweka wajibu kwa mchimbaji mdogo wa madini kama
mwajiri wa kukata kodi ya mapato ya ajira kutoka kwa
wafanyakazi wake pale tu madini yatakapokuwa
yamepatikana na kuuzwa katika masoko ya madini;
(d) Kuweka muda maalum wa kulipa kodi ya zuio ya ajira
kuwa ni wakati mchimbaji mdogo anapouza madini na
kulipa mrabaha katika masoko ya madini au vituo vingine
vya uuzaji na ununuzi wa madini vinayotambuliwa na
Tume ya Madini; na35
(e) Kuweka kiwango cha kodi cha mapato ya ajira (PAYE) cha
asilimia 0.6 ya thamani ya mauzo ya madini ambayo
italipwa na mwajiri (mchimbaji mdogo wa madini) kwa
niaba ya wafanyakazi wake.
Lengo la mapendekezo haya ni kurahisisha utozaji na ulipaji wa kodi
kutoka kwa wachimbaji wadogo wa sekta ya madini ili kuongeza
mchango wa kodi ya mapato kutoka kwenye sekta hiyo. Hatua hizi
kwa pamoja zinatarajia kuongeza mapato ya Serikali shillingi
milioni 29,776.14
C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147

59. Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa kifungu cha 124(2) cha
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, marekebisho ya viwango maalumu vya
ushuru wa bidhaa (specific duty rates) kwa bidhaa zote zisizo za
petroli yanaweza kufanyika kila mwaka ili kuvihuisha na mfumuko
wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla. Hata hivyo, kutokana
na biashara za bidhaa hizi kuzorota kutokana na athari za kiuchumi
zilizosababishwa na ugonjwa wa UVIKO-19, napendekeza
kutofanya mabadiliko ya viwango maalumu vya ushuru wa
bidhaa kwa bidhaa zote zisizo za petroli isipokuwa vinywaji
vikali na bia zitakazotengenezwa kwa kutumia shayiri
iliyozalishwa hapa nchini.

60. Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanya marekebisho
ya Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zifuatazo:

(i) Kupunguza Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa
kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini kutoka shilingi
765 kwa lita za sasa hadi shilingi 620 kwa lita. Lengo la
mapendekezo haya ni kuchochea kilimo cha shayiri hapa
nchini;36
(ii) Kuanza kutoza Ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nyuzi
na kamba za plastiki (synthetic fibres) zinazoingizwa kutoka nje
ya nchi au kuzalishwa hapa nchini zinazotambuliwa kwa
heading 55.11 na 56.07 isipokuwa zile zinazotumika kwenye
Uvuvi (HS Code 5607.50.00). Lengo la marekebisho haya ni
kulinda mazingira na kuchochea uzalishaji na matumizi ya
bidhaa za katani. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya
Serikali kwa shilingi milioni 2,644; na
(iii) Kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia
10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka 3
zinazoingizwa nchini zinazotambuliwa kwa HS Code 8711.
Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti uingizaji wa pikipiki
chakavu na kulinda mazingira. Hatua hii inatarajiwa kuongeza
ya mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 263.7.
Hatua za kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli
kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa
kiasi cha shilingi milioni 2,907.7.
D. Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2004

61. Mheshimiwa Spika, Kikao cha Mawaziri wa Fedha wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti (EAC PreBudget Consultative Meeting of Ministers of Finance) kilichofanyika
tarehe 7 Mei 2021 mjini Arusha, kilipendekeza kufanya marekebisho
ya Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha (EAC-Co