Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 04Article 541093

Burudani ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

AY kuwarudisha wasanii Mkuranga

AY kuwarudisha wasanii Mkuranga AY kuwarudisha wasanii Mkuranga

MWANAMUZIKI nguli wa kizazi kipya Ambwene Yessaya ‘AY’ ameahidi kuwarudisha wanamuziki wenzake kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.

AY ambaye ni balozi mpya wa wasanii wa fani mbalimbali aliwawakilisha Joseph Haule ‘Profesa J’, Fareed Kubanda ‘Fid Q’,Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ alisema kijiji cha wasanii kitawakomboa wasanii ikiwa wataamua kuwekeza.

"Mimi na wasanii wenzangu tulikuwa waanzilishi wa kijiji hiki (2010) miaka kumi iliyopita tulijisahau lakini sasa tunarudi kwa nguvu zote kuhakikisha yale tuliyoyaanzisha tunayasimamia," alisema AY.

Akizungumza ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Mkurunga, Filbert Sanga aliahidi kutimiza ahadi kwa kijiji cha wasanii kwa kuweka miundombinu ya barabara na umeme.

Sanga alisema wilaya hiyo itahakikisha inatoa ushirikiano kwa wasanii na jamii.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (Shiwata), Deo Kway alisema mtandao huo umeanza kutoa maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya wawekezaji wa sanaa mbalimbali.

Alisema Shiwata mbali ya wasanii na wanachama kukamilisha ujenzi wa nyumba zaidi ya 250 pia wanatarajia kujenga ukumbi wa kisasa utakaoingiza watu 2,000.

Naye mwigizaji Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ aliwashauri wasanii wanachama wa Shiwata waliofanikiwa kimaisha kurudi kuwekeza kijijini hapo kwa kujenga hosteli ili wasanii wapate mafunzo na kuandaa chipukizi wapya wa baadaye.

Join our Newsletter