Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 22Article 573364

Burudani of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Adele aitaka Spotify kuacha kuchanganya mpangilio wa albam

Adele aitaka Spotify kuacha kuchanganya mpangilio wa albam Adele aitaka Spotify kuacha kuchanganya mpangilio wa albam

Mwimbaji star wa Pop Adele ameishawishi Spotify kuondoa kitufe cha kuchanganya (shuffle) muziki kwenye albamu zote ili nyimbo zicheze katika mpangilio rasmi wa msanii.

Mwimbaji huyo alitweet: "Hatuundi albamu kwa uangalifu mkubwa na kufikiria katika orodha ya nyimbo zetu bila sababu.

"Sanaa yetu inasimulia hadithi na hadithi zetu zinapaswa kusikilizwa jinsi tulivyokusudia. Asante Spotify kwa kusikiliza."

Ndani ya muda mfupi tu Spotify walimjibu "chochote kwa ajili yako" na ikaondoa kitufe cha kuchanganya muziki kwa wasikilizaji hivyo kufanya muziki unaochezwa kwenye albamu kwenda kwa mpangilio uliopangwa na msanii.

Adele's 30 ni albamu yake ya kwanza baada ya ukimya wa miaka sita inapatikana Spotify baada ya kuachiwa rasmi Ijumaa November 19, 2021.

30 inakua albamu iliyouzwa kwa kasi zaidi katika historia ya muziki nchini Uingereza, baada ya kufikisha zaidi ya nakala 800,000 katika wiki yake ya kwanza.