Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 08Article 561973

Mitindo/Urembo of Friday, 8 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Agoma kwenda Miss World kisa Chanjo

Miss Uholanzi 2021, Dilay Willemstein Miss Uholanzi 2021, Dilay Willemstein

Mshindi wa Taji la Miss Uholanzi 2021, Dilay Willemstein ambaye alipaswa kwenda Nchini Puerto Rico December mwaka huu kushiriki shindano la Miss World 2021 amegoma kwenda kuiwakilisha nchi yake katika Fainali hizo kwasababu moja ya vigezo ni lazima Mshiriki awe amechanjwa chanjo ya corona kitu ambacho hayupo tayari kukifanya kwa sasa.

Dilay mwenye umri wa miaka 21 amesema hakujua kuwa ili uende kwenye Fainali za Miss World ni lazima uwe umechanja lakini baada ya kuambiwa ameona ni bora asiende hivyo aliyeshika nafasi ya pili kwenye mashindano ndiye atayekwenda kuwakilisha kwenye Mashindano ya Miss World.

Kupitia Instagram akaunti yake, Dilay ambaye licha ya kuwa Mwanamitindo pia nia Dancer na Mwimbaji amesema hayupo tayari kuchanjwa kwa sasa na kusema hata kama hiyo ilikuwa ni sehemu ya kutimiza ndoto zake hajutii uamuzi wake kwa kuwa afya yake ni bora kuliko chochote.