Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 05Article 541174

xxxxxxxxxxx of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Album ya Maua Sama yanukia

Huwenda mwimbaji wa Iokote, Maua Sama yupo mbioni kuachia album mpya hivi karibuni hii ni mara baada ya kuwapa uhuru mashabiki na wadau wa muziki kupendekeza jina la album yake.

Submitted by Telesphory on Jumamosi , 5th Jun , 2021 Msanii Maua Sama

Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram nyota huyo ameandika “comment jina nzuri la album” ikiwa ni kiashiria tosha kuwa huwenda tayari album inaweza kuwa imekamilika kwa asilimia kubwa.

Endapo atafanikiwa kuachia album , basi itakuwa ni ya kwanza tangu alipoingia rasmi kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva alichodumu kwa kipindi kisichopungua miaka 6.

Join our Newsletter