Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 05 29Article 540487

Burudani of Saturday, 29 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ali Kiba mbioni kuandaa albam

Ali Kiba mbioni kuandaa albam Ali Kiba mbioni kuandaa albam

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba amesema huu ni muda muafaka kwake kuachia wimbo mpya sambamba na albam.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’ nyota huyo aliandika ujumbe kuwajulisha mashabiki zake kuhusu ujio wa kazi mpya.

“Ngoma + albam uko tayari?” ndivyo alivyoandika ujumbe huo kuwaeleza mashabiki wake kama wako tayari kwa ujio huo.

Nyota huyo mkongwe kwa sasa anavuma na wimbo mpya wa ushirikiano wa Cheketua alioshirikishwa na Elias Barnabas.

Ujio wa albam yake huenda ukawa ni kitu kipya kwake kutokana na wasanii wengi kwa sasa kila mmoja kufanya kitu cha namna hiyo.

Tayari mpinzani wake mkubwa katika sanaa hiyo Nassibu Abdul ‘ Diamond Plutnumz’ amejichimbia mahali kukamilisha ujio wa albam mpya.

Mbali hao, baadhi ya wasanii waliokwishatoa albam ni Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny ikiitwa Sound from Afrika ’, Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ Definition of love, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’ Asante mama.

Join our Newsletter