Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 07 16Article 547240

Burudani of Friday, 16 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ally Kiba balozi wa Power Horse

Ally Kiba  balozi wa Power Horse Ally Kiba balozi wa Power Horse

MSANII wa kizazi kipya Ally Kiba, ametangazwa ramsi kuwa balozi wa kinywaji kuongeza nguvu mwilini ‘Energy drink’ cha Power Horse.

Akizungumza leo Ally Kiba alisema amejiridhisha na amefurahishwa kuwa balozi wa Power Horse.

“Mimi ni msanii, mimi ni mwanamichezo, ninawajibika kwenye majukumu mbalimbali ya kitaifa na kifamilia, kuna muda nachoka nahitaji nguvu za ziada, nimewaletea nguvu ya farasi mjionee,”alisema

Alisema anatembelea kauli mbiu ya Hayati Rais John Magufuli, ya kuchapa kazi, hivyo kinywaji hicho kinamsaidia kumuwezesha kuchapa kazi bila kuchoka.

Na kuhusu uwepo wa logo ya Manchester City katika kinywaji hicho, Alikiba amesema ni kwa Sababu Power Horse ni wadhamini wa team hiyo, hivyo ameahidi siku moja mashabiki wa soka kuwanoa wachezaji wa Manchester City wanakuja nchini.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Power Horse nchini, Ben Wilson alisema Ally Kiba amekuwa balozi wa bidhaa ambayo ni kubwa duniani, na imeshatambulishwa katika nchi za Nigeria, Uganda, Dubai , Djibout na sasa ni zamu ya Tanzania.

“Tunaaidi kupitia bidhaa hii, hatutawaangusha wanamichezo na wasanii, tutahakikisha tunagusa wapenzi wote wa hatutawaangusha,” alisema.