Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 08Article 584188

Burudani of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Aunt: Tunaowachekea Ndio Vivuruge Wakubwa Hapa Mjini

Aunt Ezekiel Aunt Ezekiel

MWANAMAMA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel @auntyezekiel anasema kuwa, watu wengi ambao ni wabaya ndiyo ambao wanamzunguka mtu na kila wakati anacheka nao kwa kuwaamini bila kujua ndiyo watakaommaliza.

Aunt anasema kuwa, amejifunza vitu vingi mno kupitia maisha yake ambayo ameishi kuwa mara nyingi watu wa karibu ndiyo wanawageuka siku hadi siku hivyo ni muhimu kubadilika.

“Mimi niliwahi kuambiwa kuwa mtu ambaye anakuumiza hatoki mbali kwa sababu mtu
wa mbali hawezi kukumaliza,bali wa karibu yako na wengi wao wanakuwa ni marafiki zetu wa kila siku hivyo tuchunge sana tunaowachekea,” anasema Aunt; mama wa watoto wawili.