Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 19Article 572689

Burudani of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Bifu Linazidi Kupamba Moto, Diamond Am-Unfollow Harmonize

Harmonize na Diamond Harmonize na Diamond

Siku kadhaa zilizopita miongoni mwa story kubwa ilikuwa kuhusu msanii na C.E.O wa Konde Music Worldwide Harmonize kumuondoa msanii na boss wake wa zamani Diamond Platnumz kwenye orodha ya wasanii aliowafuata (follow) kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Sasa rasmi #Diamond Platnumz na yeye amemuondoa Harmonize kwenye orodha ya watu aliowafuata (following) kwenye ukurasa wake wa Instagram, amebakiza watu 1,140 aliowafata kwenye Instagram.

Hii imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Harmonizekuongea na wanahabari katika Uwanja wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akirejea kutoka Marekani na kueleza kilichosababisha yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond.