Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 15Article 585955

Burudani of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Bryson Ndiye Mshindi wa BSS 2021/22

Bryson Ndiye Mshindi wa BSS 2021/22 Bryson Ndiye Mshindi wa BSS 2021/22

Mshiriki kutoka Dar es salaam, Brayson Yohana ameibuka Mshindi wa Mashindano ya 12 ya Bongo Star Search na kukabidhiwa Tsh. Milioni 20 na zawadi nyingine mbalimbali kutoka kwa Wadhamini tofauti ikiwemo ofa ya kuishi bure kwa mwezi mzima kwenye appartment za Palm Village.

Zawadi hizo amekabidhiwa mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Mechezo Mohamedi Mchengwera ambaye pia ameipa Uongozi wa BSS Tsh. Milioni 5 kama sehemu ya kuwaunga mkono Kwenye kuibua vipaji.