Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 20Article 573043

Burudani of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Burna Boy Amposti Harmonize

Burna Boy na Harmonize Burna Boy na Harmonize

Miongoni mwa stori zinazotrendi ni kitendo cha staa wa muziki wa Nigeria, Burna Boy kumposti msanii wa Bongo Fleva, Harmonize au Konde Boy Mjeshi na kuweka ishara ya kopa jekundu kwa maana ya upendo.

Jambo hilo limetokea siku moja baada ya Harmonize kufunguka mengi ikiwemo ishu ya kuzuiwa na Diamond kupanda stejini kwenye shoo ya Burna Boy nchini Rwanda miaka kadhaa iliyopita.

Hii inaonesha upendo wa Burna Boy kwa Harmonize au Teacher Konde bado ni 100%.

Kwa mujibu wa Harmonize, wawili hao tayari wamefanya kolabo za nyimbo 4, lakini zilozotoka ni mbili tu.