Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 05Article 541114

xxxxxxxxxxx ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dayna Nyange aanza kupokea oda

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dayna Nyange amesema tayari ameshaanza kupokea majina ya watu ambao wanahitaji kupata albamu fupi ‘EP’ ya Elo ambayo itakuja hivi karibuni.

Dayna Nyange amezidi kuwasha moto juu ya albamu hiyo kwa kumshirikisha mwanamuziki Davido kutoka nchini Nigeria, ambaye amemshirikisha katika wimbo wa Elo ambao ndiyo uliobeba jina la albamu hiyo.

Kwa mwanamuziki Dayna Nyange hii itakuwa albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki nwaka 2013, ambapo pia amefanya kazi kubwa na nzuri, ikiwemo ile ya Komela.

Wanamuziki wengi kwa sasa wamejikita katika utoaji wa albamu katika mfumo mtandao baada ya soko la Cd kuvamiwa na watu ambao wamekuwa wakionekana kama wakidurufu na kufanya wasanii wasipate mafanikio.

Join our Newsletter