Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 13Article 562996

Burudani of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Diamond Ana Mlima Mrefu AFRIMMA

Diamond Platnumz Diamond Platnumz

Tuzo za AFRIMMA kwa mwaka 2021, zina ushindani mkubwa mno, pana mlima mrefu ambao inabidi msanii aupande ili kutwaa tuzo hiyo.

Ushindani ambao wengi wanasema si ajabu wasanii wa Bongo Fleva wakaambulia patupu.

Wapo wanaosema kuwa, hata kwa Diamond ambaye anategemewa na mashabiki wake afanye vizuri, kuna kila dalili akapita kwenye mtihani mzito kwenye tuzo hizo pale tu itakapotokea akaambulia patupu kama ilivyotokea kwa zile Tuzo za BET.

Kila kipengele alichoingia Diamond, kina wasanii wakubwa Afrika ambao kila siku wanasikika wakivunja na kuweka rekodi mpya kwenye kiwanda cha muziki wa Afrika.

Katika tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika Novemba 14, 2021, Diamond anawania Kipengele cha Msanii Bora Afrika ambapo amekutana kwa mara nyingine Burna Boy (Nigeria), Fally Ipupa (DR Congo), Wizkid (Nigeria), Aya Nakamura (Mali), El Grande Toto (Morocco), Tay C (Cameroon) na Dadju (DR Congo).

Hapa unaona anakutana tena na Burna Boy, Wizkid na Nakamura ambao walipepetana kwenye Tuzo za BET halafu Burna Boy akatwaa tuzo hiyo.

Pia hapo wameongezeka wakali kama Fally Ipupa, Grande Toto, Tay C na Dadju ambao nao muziki wao siyo wa kitoto.

Ni kweli akishindwa yeye ni Tanzania inashindwa kwa sababu anaiwakilisha nchi, lakini penye namba au takwimu, lazima kuwe na tahadhari na siyo kupeana maneno matamumatamu tu, lazima kuwe na mikakati ya kushinda.

Lakini kama Watanzania wasipoambiana ukweli, muziki wa Tanzania utakwenda kupata aibu kwa mara nyingine kama ilivyokuwa kwenye BET.

Tusijisahaulishe kwamba, nafasi anayowania Diamond ni kubwa mno; yaani NI MSANII BORA WA AFRIKA!!! Tuamke!