Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 05Article 555385

Burudani of Sunday, 5 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Diamond ayakumbuka mahaba ya Wema Sepetu

Diamond ayakumbuka mahaba ya Wema Sepetu Diamond ayakumbuka mahaba ya Wema Sepetu

Staa wa muziki nchini Tanzania Diamond Platnumz amefunguka kwamba kila akiitazama video ya wimbo mpya ya naanzaje anakumbuka mahaba mazito ya Madam akimaanisha Wema Sepetu.

Diamond ameshea hilo akipromote video yake hiyo kwenye mtandao wa Instagram kisha akaandika maneno yafuatayo

"Nikiitazama hii video, hususan kipande hiki nakumbuka mbali sana...enzi za mahaba mazito na Madam, enzi ambazo tulikuwa tunajifungia chumbani wiki nzima, nakwepa ku-record na hata show ikitokea naitaftia sababu ya kutokuwepo"

"Kiukweli wimbo huu wakati nautoa sikuuchukulia serious, niliutoa tu kama 'bonus' kwa kujua mashabiki zangu wameni-miss kunisikia nikiimba hivyo licha ya kupokelewa na kupendwa sana ulivyotoka"

"For some reason kadri muda uendanvyo nimejikuta naupenda sana mbaya zaidi kila niusikiapo unanifanya nitamani tena kumpenda mtu na kuwa tena wenye mahusiano japo ghafla akili timamu hunijiagna kunambia Simba jifocusie zako kwenye kazi mwaya"

Couple ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu ni moja kati ya couple iliyokuwa gumzo nchini Tanzania ambayo ilianza mwaka 2010 na kuachana 2014.