Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 25Article 574057

Muziki of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Dimpoz kuachia ngoma na Fally Ipupa

Ommy Dimpoz akiwa studio na Fally Ipupa Ommy Dimpoz akiwa studio na Fally Ipupa

Baada ya kuwepo kwa Story za Chini Chini Kuhusu kuwepo kwa ngoma ya Pamoja kwa wakali wa Muziki Afrika, Omary Nyembo "Ommy Dimpoz" Pamoja na nguli wa muziki wa Rhumba kutoka Jamhuri ya Congo Fally Ipupa N'simba "fally Ipupa" Ni wazi sasa Kuwa Kolabo hiyo imekamilika Na huenda ikatoka siku za hivi karibuni.

Dimpoz ameshare taarifa hiyo katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, kwa kupost picha akiwa Studio na mhuyo na kisha kusindikiza na Caption yenye maneno;

"Haya viuno vyenu vitieni grisiii Mapemaaa" kisa akamaliza na emoji za kicheko kuonesha ishara ya furaha.

Hatua hii ya Ommy Dimpoz ni kama kuwaweka sawa watanzania kwa kuhakikisha wanajiandaa kusikiliza ushirikiano baina ya hao watu wawili.

Ommy Dimpoz ameshafanya Colabo kadhaa na wasanii wa Kimataifa kama vile J. Martins kutoka Nigeria, Seyi Shay na wengine wengi hivyo hii ni miongoni mwa muendelezo wa kile alichoanza hapo awali.