Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 21Article 573175

Burudani of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Drake na Kanye kwenye steji moja December

Drake na Kanye Drake na Kanye

MARAPA wa kiwango cha Dunia, Drake na Kanye West kutoka Marekani, sasa uhusiano wao ni kizazi sana baada ya kumaliza bifu lao.

Drake na Ye wameungana tena ambapo Kanye ameposti picha akiwa na Drake nyumbani kwake huku Kitaa cha Toronto nchini Marekani.

Taarifa za ndani kabisa zinasema kuwa wamemaliza tofauti zao baada Kanye kutamani wapatane kwa muda mrefu. Drake na Kanye waliingia kwenye bifu kubwa baada ya Kanye ku-tweet karibia Tweets 25 akidiss na kumponda Drake kwa kile ambacho Kanye hakuwahi kufunguka sababu ilikuwa ni nini.

Ugomvi wao ulikua mkubwa zaidi baada ya Drake kutangaza kutoa album yake "Certified Lover Boy" siku ambayo Kanye alikua akiachia album ya Donda.

Hivi karibuni kwenye mahojiano na Noriega kupitia podcast ya Drink Champs, Kanye alisema yuko tayari kupanda kwenye steji za Verzuz kuchuana na Drake lakini aongezewe wasanii wengine wanne.

Tayari Drake na Kanye wametangaza kukutanga stejini Tarehe 9 December ndani ya ukumbi wa L.A. Coliseum jijini Los Angeles, California.