Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 12Article 585268

Burudani of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Dulla Makabila: Nimetulia Kwenye Ndoa

Dulla Makabila: Nimetulia Kwenye Ndoa Dulla Makabila: Nimetulia Kwenye Ndoa

MWAMBA aliyejipa taito ya Mfalme wa Singeli, Abdallah Mzee almaarufu Dulla Makabila amefunguka kuwa, kwa sasa ameamua kutulia na mkewe wa ndoa aitwaye Rahma.

Dulla Makabila anasema kuwa, kwa sasa ameamua kutulia na Rahma hivyo skendo za kuwa na wanawake wa nje ya ndoa kwake anazipa kisogo.

“Kwa sasa mke wangu, Rahma hayupo nchini, yupo nje ya nchi kikazi, lakini namuheshimu sana na ninampenda kuliko maelezo, pia namuahidi kumsheshimu na kumjali, nimetulia kwenye ndoa yangu, sina haja ya kuwa na mwanamke mwingine, nitamsubiri hadi atakaporejea Bongo,” anasema Dulla Makabila ambaye hivi karibuni alizawadiwa gari na mkewe huyo.