Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 07Article 541549

Burudani of Monday, 7 June 2021

Chanzo: eatv.tv

"EP imenunuliwa kwa Milioni 1" - Marco Chali

"EP imenunuliwa kwa Milioni 1" - Marco Chali

Producer Marco Chali amefunguka kusema bado hajapanga bei ya mauzo ya Extended Playlist (EP) yake ya Ona ila tayari kuna ndugu yake ameshainunua kwa Tsh Milioni moja na Laki saba, pia wapo walionunua kwa Tsh Laki Tano hadi Nne.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumatatu , 7th Jun , 2021 Picha ya Producer Marco Chali

Akizungumza kwenye show ya PlanetBongo ya East Africa Radio Marco Chali amesema hata mtu akija na Tsh mia tano watamuuzia EP hiyo kwa sababu wanataka ku-balance kwa kila mtu.

"Mpaka sasahivi sijapanga bei ya EP yangu ila kuna ndugu yangu ameshainunua kwa shilingi Milioni 1 na laki 7 kuna walinunu kwa Laki 5 wengine Laki 4, hata akitokea mtu anataka kwa Jero tutamuuzia maana tuta-balance" 

"Unapojaribu kufanya muziki unahitaji watu wenye uelewa wa muziki ndio maana nilipofanya EP yangu niliwaita wadau wa muziki, nashukuru mungu 'feedback' yao ilikuwa nzuri sana" ameongeza Marco Chali 

Join our Newsletter