Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 23Article 559195

LifeStyle of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Exclusive:Wafunga Ndoa wodini baada ya mume kupata ajali na kukatwa mguu (video+)

Exclusive:Wafunga Ndoa wodini baada ya mume kupata ajali na kukatwa mguu (video+) play videoExclusive:Wafunga Ndoa wodini baada ya mume kupata ajali na kukatwa mguu (video+)

Ndoa ya kijana Augustine Makule na mpenzi wake Rose Kimaro imevuta hisia za wengi jijini Dodoma baada ya wawili hao kufunga ndoa wodini. Hatua hiyo imekuja baada ya Bwana harusi kupata ajali ya Bodaboda siku mbili kabla ya siku ya ndoa yao.

Ajali hiyo ya pikipiki iliyotokea eneo la zuzu Dodoma imepelekea kijana Agustino kukatwa mguu wake wa kulia na vidole vitatu vya mguu wake wa kushoto.

Licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo waliamua kuendelea na ratiba yao ya ndoa ambayo waliifungia ndani ya wodi ambapo mchungaji alifika na baadhi ya waumini na kuendelea na taratibu za ndoa.