Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 15Article 586018

Burudani of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Fahyma: Kila mtu anaachika

Fahyma na Rayvanny Fahyma na Rayvanny

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Faima Msenga almaarufu Fahyma anasema kuwa, anajijua yeye ni mrembo mno, lakini suala la kuachana au kuachwa na mwanaume ni la kila mtu hivyo watu waache kuropoka.

Mwanamama huyo anasema kuwa, kuna watu wengi huwa wanakomenti mambo ambayo hayana maana kwenye picha zake, wakijua watamuumiza, lakini wapi.

Anasema kuwa, mara utasikia mtu akisema kama ni mrembo kwa nini ameachwa, lakini anachojua ni kwamba kama mapenzi yakifika mwisho watu huachana tu na hata wawe wazuri kama malaika.

“Binafsi najijua kuwa ni mzuri, tena sana, sasa nawashangaa hao ambao huwa wanakuja kwenye akaunti yangu kunitukana kuwa kama mimi ni mrembo, kwa nini sipo na baba wa mtoto wangu, wanasahau kuwa kuna muda mapenzi huwa yanaisha na yakiisha lazima kila mtu aendelee na maisha yake. Mtu hata uwe mzuri kama malaika, kama upendo haupo tena ni haupo tu,” anasema Fahyma ambaye ni baby mama wa msanii Rayvanny.