Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 10Article 584758

Burudani of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Fahyma: Naumwa Jamani

Fahyma na Rayvanny Fahyma na Rayvanny

BABY mama wa msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Faima Msengi almaarufu Fahyma, ameibua mshtuko miongoni mwa wafuasi wake kwenye mitandao tofauti ya kijamii baada ya kusema anaumwa.

Kwa mujibu wa Fahyma, anaumwa sana, jambo ambalo wafuasi wake hawawezi kuacha kulizungumzia huku wengine wakimuombea na kumtaka aendele hospitalini kwa matibabu ya haraka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

“Naumwa jamani!...” Ameandika Fayhma.

Taarifa hiyo ya Fahyma kuumwa imesambaa kwa haraka kwenye mitandao tofauti ya kijamii na kuzua hisia tofauti.

Wafuasi wake wamekuwa wakimuuliza Fahyma kwa nini anaumwa huku wengine wakionesha hisia za kufurahishwa na taarifa hiyo.

Rayvanny na Fahyma walitengana mapema mwaka jana huku kutengana kwao kukizua kizaazaa baada ya jamaa huyo kuruka kimapenzi na Paula Kajala ambaye ni mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja na Prodyuza P Funk Majani.