Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 13Article 585460

Burudani of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Grammy kufanyika Aprili

Grammy kufanyika Aprili Grammy kufanyika Aprili

Taarifa mpya ni kuwa hafla ya utolewaji wa Tuzo za Grammy 2022 zitafanyika kati ya Aprili 3 au 10, mwaka huu baada ya awali kuahirishwa kufanyika Januari 31.

Wiki iliyopita ilitolewa taarifa ya kuahirishwa kufanyika kwa tuzo hizo kutokana na tishio la ongezeko la virusi vipya vya Omicron, lakini sasa hafla hiyo inaweza kufanyika Aprili kwenye Ukumbi wa Staples Centre, Los Angeles, Marekani.

Hii inakuwa mwaka wa pili mfululizo kwa tuzo hizo kuahirishwa tarehe yake iliyopangwa awali toka Januari na kufanyika Machi 14, 2021 kutokana na Covid-19.

Hata hivyo, bado haijaelezwa kama kuna mabadiliko mengine ya ratiba ya hafla hiyo itakayoshereheshwa na mchekeshaji, Trevor Noah ambaye alifanya hivyo pia kwenye hafla ya tuzo hizo mwaka jana.