Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 30Article 560602

LifeStyle of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Gumzo!!Samaki wa ajabu anaepaa aonekana Dar es Salaam

Gumzo!!Samaki wa ajabu anaepaa aonekana Dar es Salaam Gumzo!!Samaki wa ajabu anaepaa aonekana Dar es Salaam

Hali isiyo ya kawaida imetokea maeneo ya Soko la samaki Msasani, inasemekana Wavuvi baadhi wameleta gumzo baada ya kudai kumwona Samaki wa ajabu mwenye uwezo wa Kupaa akiwa baharini.

Ili kujua Zaidi kuhusiana na story hii team yetu ilifika Soko la Samaki maeneo ya hayo na kuongea na Wavuvi wanaodai kumuona Samaki huyo.

Kujua Zaidi tulipata nafasi ya kuongea na Mvuvi anaejulikana kwa Jina la Mkojani, huyu ni mmoja wa wavuvi wanao semekana kumwona Samaki huyo wa ajabu. Swali tulilomuuliza ni je, hii ni mara ya kwanza ya wao kumuona huyo Samaki au alishawahi kuonekana zamani?

“Kusema kweli kwangu mimi binafsi hii ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kumwona au kujua kuna Samaki kama huyo, na ndio maana nilivyomuona nilishituka na kustaajabu”.

Swali lingine lilikuwa je walifanikiwa kumvua huyo Samaki? “Hapana bro, tulijitahidi kufanya hivyo sema alitushinda ujanja, sema mimi na wenzangu tumepanga kurudi tena sehemu ile ile tuliyomwona tuone kama tunaweza kubahatika tena kumwona na ikiwezekana kumvua”.

Kufuatilia story hii unaweza kubofya kwenye video hapo chini/juu kujua Zaidi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by CR millard ayo (@millardayo)