Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 12Article 585196

Burudani of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Hali si Shwari Lebo ya Konde Music Worldwide

Hali si Shwari Lebo ya Konde Music Worldwide Hali si Shwari Lebo ya Konde Music Worldwide

BAADA ya uongozi wa Lebo ya Konde Music Worldwide almaarufu Konde Gang iliyo chini ya Harmonize kutangaza kumalizika kwa mkataba na msanii wake Country Wizzy, imeelezwa hali si shwari ndani ya lebo hiyo.

Konde Gan ndiyo walioanza kutoa taarifa hii ndipo yakaibuka mambo mengi; “Taarifa; Mkataba kati ya Konde Music Worldwide na Country Wizzy umemalizika hii Tar 8 Januari 2022. Kuanzia leo (jana) Country Wizzy atakuwa msanii anayejitegemea baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili.

“Konde Music Worldwide inamtakia kila lenye kheri Country Wizzy kwenye career yake ya music pamoja na maisha kwa ujumla. All the best Wizzy!”

Baada ya taarifa hiyo ndipo akaibuka mtu aliyejitambulisha kama mwanasheria wa Country Wizzy aitwaye Nictagon Nicky na kusema; “Mkataba umemalizika? Muda umeisha? Pande zote zimefikia makubaliano? Kipi ni kipi?

Katika usitishwaji wa mkataba baina ya pande mbili, haki na taswira (chapa) ya kila upande lazima ilindwe, isionekane mmoja ndiye amemuacha mwingine…” Wakati kukiwa na utata huo, madai mengine mazito yanayovumishwa yanadai kuwa, wasanii wengine wawili ndani ya lebo hiyo, Cheed na Killy wapo mbioni kutimka Konde Gang ila mikataba inawabana, wanatakiwa kulipa mamilioni ili kuvunja mikataba.

Country Wizzy aliingia Konde Gang akitumia jina la Country Boy na amedumu kwenye lebo hiyo yapata mwaka mmoja tu.