Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 12Article 585265

Burudani of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Hamisa: Mwaka huu sifanyi makosa

Hamisa Mobetto Hamisa Mobetto

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Hamisa Mobeto anasema kuwa, mwaka huu wa 2022 hataki kufanya makosa ya kutumia pesa hovyo, bali anataka azitumie katika mambo ya msingi.

Hamisa ambaye ni msanii wa Bongo Fleva mwenye figa matata anasema kuwa, 2022 anataka awekeze pesa zake katika ujenzi na siyo starehe kama ilivyokuwa mwaka 2021.

“Unajuu mwaka huu siyo kama 2021 ambao sikufanya mambo mengi ya maana, lakini pesa nyingi nilizitumia kwenye starehe zaidi, ndiyo maana namuomba Mungu anijaalie uzima mwaka mwaka huu sitaki kufanya makosa, nataka nifanye mambo ya muhimu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwekeza kwenye ujenzi tu na siyo kupati (party) kila siku,” anasema Hamisa ambaye mwaka jana alifanya vizuri mno na ngoma yake ya EX-Wangu Remix.