Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 07 13Article 546892

Burudani of Tuesday, 13 July 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hamisa akaribia kumng’oa Zuchu, awasukuma Diamond na Alikiba

Waziri Kitila atoa ufafanuzi sanamu la Magufuli Sabasaba Waziri Kitila atoa ufafanuzi sanamu la Magufuli Sabasaba

Hamisa kumng’oa Zuchu sasa. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya huko  kwenye mtandao wa YouTube nyimbo zao kuchuana vikali.

Nyimbo hizo ni Nyumba Ndogo ambayo ni ya Zuchu iliyotoka wiki moja iliyopita na ile ya X Wangu ya Hamisa iliyotoka siku nne zilizopita.

Kwani mpaka sasa mpambano unasema Nyumba ndogo inakamata namba moja na tayari umetazamwa zaidi ya mara milioni nne.

Huku X wangu wa Hamisa wimbo aliourudia wa msanii Seneta Kilaka na kushirikiana kuimba natye ukikamata namba mbili ukiwa na umetazamwa zaidi ya mara milioni moja.

Wakati hali ikiwa hivyo, nafasi ya tatu inakamatwa na Ali Kiba na wimbo wake wa  Salute alioimba kwa kushirikana na msanii kutoka nchini  Nigeria, Rude Boy huku namba nne ikishikiliwa na Diamond kwa wimbo wake wa Kamata.

Nyimbo hizo za mahasimu wakubwa katika muziki wa Bongofleva, wiki iliyopita zikulikuwa zikichuana katika namba moja na mbili lakini ndio hivyo Hamisa ni kama kazisukumilia mbali.

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Maoni