Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 03Article 540721

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Hamisa apaki mabegi kumfuata Rick Ross

Ni Headlines za msanii wa filamu Hamisa Mobetto ambaye amemjibu staa wa muziki wa HipHop duniani Rick Ross, kwamba yupo tayari kuhamia nchini Marekani.

Rick Ross amepita kwenye ukurasa wa Instagram anaoutumia Hamisa Mobetto kisha ku-like na ku-comment kwa kumuuliza kwamba, 'unahamia America'?

Hamisa Mobetto akamjibu kwa kuandika "Nimeshapaki mabegi yangu yote, nipo tayari". 

Hii sio mara ya kwanza kwa Rick Ross kutembelea ukurasa wa Hamisa Mobetto kwani ya siku ya Aprili 29, msanii huyo alipita kwenye page ya Hamisa kwa ku-like na ku-comment 'emoj' ya nyota kwenye picha ya Hamisa kisha Hamisa akamjibu kwa 'emoj' ya moto.

Pia siku ya Mei 19 Rick Ross alipita tena kwenye ukurasa wa Hamisa Mobetto kwa ku-like na ku-comment kwa mara nyingine.

Kwa ilivyo kwa sasa Rick Ross anaonekana kuvutiwa na post staa wa filamu Hamisa Mobetto baada ya kutembelea page yake mara kwa mara.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.

Join our Newsletter