Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 22Article 573481

Burudani of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Harmonize Apewa Ubalozi wa Usafi Dar

Harmonize Harmonize

Supastaa wa Bongo Fleva, Harmonize amesema kutokana na vijana wengi kumfuatilia kama msanii mkubwa na kioo cha jamii, sasa jukumu lake kuhamasisha suala la usafi katika jiji la Dar es Salaam.

Harmonize amesema leo Jumatatu, Novemba 22, 2021 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi jijini Dar inayosimamiwa na Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla na kumpongeza pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazo fanya ili kuifanya Tanzania kuwa bora.

Harmonize ambaye ni Balozi wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira Mkoa wa Dar, amesema;

"Ningependa kuwahimiza vijana kwamba usafi ni suala letu la msingi, na najivunia kuwa kati ya vijana wanaohimiza usafi kwani ni haki yetu ya msingi" Harmonize.

Mbali na Harmonize, wasanii wengine wakubwa waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ni Alikiba, Steve Nyerere pamoja na Viongozi wengine wa Kiserikali wakiwemo Wakuu wa Wilaya.