Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 18Article 572578

Burudani of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Harmonize: Diamond Alisema Simuwezi Kihela, Serikali, Kiuchawi

Harmonize na Diamond Harmonize na Diamond

MWANAMUZIKI Harmonize, leo Alhamisi, Novemba 18, 2021 amerejea nchini akitokea Marekani alipokwenda kufanya shoo zake baada ya kutua nchini ameongea na wanahabari katika Uwanja wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kueleza sababu zilizosababisha yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond Platnumz.

“Nilimfuata Diamond nikamwambia tatizo ni nini mimi na wewe tunagombana? Akasema hivi: ‘Mimi nikimpa mtu heshima yangu, kama hatanirudishia naichukua kinguvu, unataka kushindana na mimi huniwezi kihela, huniwezi kiserikali, huniwezi kichawi nipe mkono tushindane’.

“Nikabaki nimezubaa, akaingia kwenye gari akaondoka. Siku iliyofuata nikaenda ofisini kwake kumuona.”

“Wakati Wasafi inaanzishwa mimi na yeye ndiyo tulikuwa tunapambania Wasafi, nilikuwa kimbelembele kusimamia vitu vingi, hata baadhi ya vifaa nilitoa mimi baada ya vya kwake kuchelewa.

“Kamati ilikuwa mimi yeye, Mustapha na mama Dangote, wakati huo hakukuwa na Babu Tale wala Sallam, wao walikuwa bize na Dizzim, kwa walikuwa hawaamini kwenye Wasafi Media.” amesema Harmonize.