Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 13Article 562999

Burudani of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Harmonize, Diamond Wanapishana Tu Marekani

Diamond Platnumz na Harmonize Diamond Platnumz na Harmonize

Diamond Platnumz, (Oktoba 8,2021) alianza ziara zake za nchini Marekani kwa ajili ya shoo ambapo atalazimika kupishana tu na msanii mwenzake, Harmonize.

Diamond alianzia shoo zake katika Ukumbi wa Buckhead Theatre huko Atalanta, Marekani ambapo Harmonize tayari amefanya yake huko Columbus, Ohio, Houston na New York tangu Agosti 15, 2021 alipoanza ziara zake nchini humo.

Kwa upande wake Diamond, baada ya shoo ya Atalanta, alikwenda Washington DCkabla ya kuelekea Seattlekisha atakwenda Minneopolis, New York, Louisville, Arizona, Houston, Boston na Dallas kisha ataendelea na shoo za Ulaya hadi mwanzoni mwa mwaka 2022.

Kwa upande wake, N’jomba Nchomali, baada ya kupitia Miji ya Columbus, Ohio, Houston na New York sasa ataendelea kukiwasha huko Los Angeles, Las Vegas, Idaho, Minnesota, Syracuse kisha atarejea New York kwa mara nyingine.