Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 05Article 561412

Burudani of Tuesday, 5 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Harmonize Jeshi la Mtu Mmoja Akiwasha Kinoma

Harmonize Harmonize

MTANDAO unaohusika na kutoa takwimu za wasanii Bongo, umetoa orodha ya wasanii kumi waliotazamwa zaidi kwenye Mtandao wa YouTube kwa Mwezi Septamba, 2021, lakini kubwa zaidi ni mjadala kwamba pamoja na kuwa yeye ni jeshi la mtu mmoja, lakini Harmonize amekiwasha kinoma.

Ripoti hizo zimeonesha Diamond Platnumz anashikilia nafasi ya kwanza huku akifuatiwa na wasanii wengine akiwemo Harmonize.

DIAMOND PLATNUMZ

Baba T au Simba wa Tandale ndiye kinara katika orodha hii. Licha ya kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na idadi ya watazamaji wengi katika mtandao wa YouTube, lakini utofauti wa idadi hiyo ni mkubwa mno ukilinganisha na wasanii, kuanzia namba mbili hadi kumi.

Pengine hii ni kutokana na kazi mzuri anazozifanya Simba zinaopeta Bongo na majuu. Lakini pia ni kutokana na nguvu kubwa anayoitumia kuvuka mipaka zaidi kwa kufanya ngoma na wasanii kibao wenye majina makubwa kimataifa. Mfano; ngoma yake ya Waah aliyomshirikisha Koffi Olomide, ambayo imemuingiza kwenye rekodi ya kutazamwa na watu wengi kwa muda mchache.

Mondi amefikisha idadi ya watazamaji milioni 38.1 kwa mwezi akiwa amemuacha Ibraah ambaye anashika nafasi ya kumi kwa watazamaji milioni 36.24!

RAYVANNY

Nafasi ya pili imekamatwa na Rayvanny au Chui ambaye anafanya kazi chini ya Diamond licha ya kuwepo kwa tetesi za kujiondoa kwenye lebo hiyo.

Huyu ni msanii wa pili kutoka WCB kutajwa katika nafasi kubwa ya wasanii waliotazamwa zaidi kwenye YouTube. Pengine ni kutokana na ukubwa wa lebo hiyo na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika kuwainua wasanii wake kimataifa.

Chui ametajwa kufikisha watazamaji milioni 21.3 akiwa amemuacha Ibraah kwa watazamaji milioni 19.44 huku akiwa amezidiwa na bosi wake kwa watazamaji milioni 16.8.

HARMONIZE

Tembo au Teacher anayesumbua kimataifa kwa ngoma zake kali na shoo za kibabe ametajwa kuwa nafasi ya tatu ya wasanii waliotazamwa zaidi kwenye YouTube.

Harmo anafungua ukurasa wa Lebo ya Konde Gang ambayo anaiongoza huku akiwa na watazamaji milioni 13.9 akiwa amemzidi kijana wake, Ibraah kwa watazamaji milioni 12.04 huku akiwa amezidiwa na Diaomond kwa watazamaji milioni 24.2.

MBOSSO

Kichwa hiki kutoka Lebo ya Wasafi ametajwa kuwa nafasi ya pili kati ya wasanii kumi waliotazamwa zaidi kwenye YouTube hivyo anakuwa msanii wa tatu kutoka lebo hiyo kutajwa kwenye listi hiyo.

Mbosso ambaye anatambulika kwa nyimbo zake za mahaba kama staa wa kihindi, anatajwa kufikisha watazamaji milioni 11.3 huku akiwa amezidiwa na Diamond kwa idadi ya watazamaji milioni 26.8.

ZUCHU

Bidada Zuhura naye kutoka Usafini anakuwa msanii wa nne kutoka lebo hiyo kutajwa katika orodha hiyo. Zuchu anatajwa kuwa na watazamaji milioni 11.1 juu ya King Kiba ambaye ana watazamaji milioni 6.1.

KING KIBA

Mfalme huyo ambaye hivi karibuni amaweka wazi ujio wa albam yake mpya ametajwa kushika nafasi ya sita kati ya wasanii kumi waliotazamwa zaidi kunako YouTube.

King Kiba anatajwa kufikisha watazamaji milioni 6.12 akiwa amezidiwa na Diamond kwa idadi ya watazamaji milioni 31.98

NANDY

Bidada Nandy ni msanii wa pili wa kike kutajwa kwenye kutoka nje ya lebo.

Nandy ametajwa kufikisha watazamaji milioni 4.28 kwenye YouTube huku akiwa ameachwa na Zuchu kwa idadi ya watazamaji milioni 6.82.

LAVA LAVA

Mr Love Bite amekuwa msanii wa tano na wa mwisho kutoka Wasafi kutajwa kwenye orodha hiyo.

Lava Lava anashikilia nafasi ya nane kwa kuwa na watazamaji milioni 3.93 kunako YouTube huku akiwa amezidiwa kwa idadi ya watazamaji milioni 34.17 na Diamond.

JUX

Jux anakuwa msanii wa pili nje ya lebo kutajwa katika orodha hiyo akiwa chini ya Nandy.

Jux anatajwa kuwa na watazamaji milioni 3.9 wa YouTube, akiwa ameachwa mbali na Diamond kwa idadi ya watazamaji milioni 34.17.

IBRAAH

Ibraah kutoka Konde Gang anafunga ukurasa wa wasanii kumi waliotazamwa zaidi YouTube kwa mwezi Septemba.

Ibraah amefikisha idadi ya watazamaji milioni 1.86 huku akiwa amezidiwa na na Jux kwa idadi ya watazamaji milioni 2.04.