Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 18Article 572584

Burudani of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Harmonize: Nafikira Kufuta Tattoo ya Diamond

Harmonize Harmonize

MWANAMUZIKI Harmonize, leo Alhamisi, Novemba 18, 2021 amerejea nchini akitokea Marekani alipokwenda kufanya shoo zake baada ya kutua nchini ameongea na wanahabari katika Uwanja wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kueleza sababu zilizosababisha yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond Platnumz.

“Walijua nikitoka nje nitakufa, waliona Rich Mavoko alivyotoka akapotea, huu mwaka wa tatu sasa na nimetoka Marekani. Kila nilichofanya wanaona nakosea, niliponunua V8 wakasema namuiga yeye.

“Mimi bado nina mheshimu Diamond, nina tatuu yake hapa mkononi sina mpango wa kufuta lakini siku zinavyoenda mbele naweza nikafuta kama mtu anatamani wewe ufe mi tabaki na tatuu ya nini?

“Maugomvi yakawa mengi, faini kila mara. Nilishawahi kupigwa faini milioni 10 kisa nimeenda uwanjani kuangalia mechi ya Taifa Stars. Nikaambiwa nilipe Sh milioni 10 na nikalipa,” amesema Harmonize.