Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 18Article 572572

Burudani of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Harmonize: Ukianza Ku-Shine Lazima Ugombane Na Diamond

Harmonize na Diamond Harmonize na Diamond

MWANAMUZIKI Harmonize, leo Alhamisi, Novemba 18, 2021 amerejea nchini akitokea Marekani alipokwenda kufanya shoo zake baada ya kutua nchini ameongea na wanahabari katika Uwanja wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kueleza sababu zilizosababisha yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond Platnumz.

“Kila mtu ana nafasi yake kwenye muziki, siyo kwa sababu nimesainiwa kwenye lebo basi niache kukimbilia ndoto zangu.

“Hakuna msanii yeyote wa Afrika ambaye amewahi kuperform MTV, inamaana Maluma alivyomchek Rayvanny na kumwambia waka-perform MTV, Rayvanny angekataa kwa kuwa Diamond hakuwepo? Rayvanny alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa anakimbilia ndoto zake.

“Mimi pia nilikuwa nakimbilia ndoto zangu, nilipofanya hivyo nilikuwa nakimbilia ndoto zangu. Wasanii wote waliogombana na Diamond ni wale ambao walikuwa chini, ukishaanza kuwa mkubwa anagombana na wewe.

“Mfano mzuri Shetta, alikuwa rafiki yake mzuri wanasaidiana mambo mengi, alivyoanza ku shine wapambe wakamwambia ‘umeona? Anakupita huyo!

“Ilikuwa hivyo pia kwa Ommy Dimpoz na wasanii wengine kibao.” amesmea Harmonize baada ya kutua Dar es Salaam, leo Alhamisi akitokea Marekani.