Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 05Article 541135

xxxxxxxxxxx of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Haromize amuelezea Killy

MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amesema ilimchukua mwaka mmoja tangu alipopewa nafasi ya kumsimamia mwanamuziki Killy ambaye alitoka King Music.

Akizungumzia juu ya mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa ametoa wimbo wake wa kwanza katika lebo ya Konde, alisema ilikuwa changamoto sana kutafuta kitu ambacho anakitaka katika muziki wake.

Alisema anaamini kila msimamizi anakuwa na mfumo wake wa kusimamia wasanii, huku akiamini msanii huyo anaweza kuleta chachu katika tasnia ya muziki Tanzania.

“Mungu kwa kutupa moyo wa subira pande zote mbili na uvumilivu yamesemwa mengi yakukatisha tamaa sijuwi kakusanya watoto wa watu na kupiga nao picha, “alisema.

Join our Newsletter