Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 10Article 542011

Burudani of Thursday, 10 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Hemed aongoza kuzindua promosheni ya Infitix

Hemed aongoza kuzindua promosheni ya Infitix Hemed aongoza kuzindua promosheni ya Infitix

KAMPUNI ya Simu ya Infinix leo imezindua promosheni yake ya Note 10 Series ambazo ni Note 10 na Note 10 Pro.

Katika uzinduzi huo Staa wa Bongofleva na Bongomovie Hemed aliongoza zoezi hilo akiwa ni Balozi wa Infitix Tanzania .

Akizungumza na wanahabari kwenye duka la Infinix lililopo Mlimani City, Manager Mauzo Infinix, Winfrida Chumi, ameeleza kuwa kwa kipindi cha muda wa wiki mbili Infinix tutakuwa na ofa maalumu kwa wateja wa Infinix NOTE 10 na NOTE 10 pro kwa wateja wa simu hizo mbili tutawazawadia game aina ya PS5, Ticket ya kwenda nyumba za Cinema na zawadi nyengine kibao.

Mkufunzi wa bidhaa za kampuni hiyo, Eda Charles akizungumzia simu hizo alianza na Note 10 Pro.

Eda amesema simu hizo zimeshinda tuzo ya Best Designer mwaka 2020/2021 kutokana na muonekano wake mzuri.

Akiielezea muonekano wa mbele Eda amesema “Note 10 Pro ina muonekano mzuri ikiwa na kamera kati yenye uwezo mkubwa kabisa wa mega pixel 16 inayomfanya mtumiaji kupata picha bora kabisa.

“Simu hii ina skiri kubwa ya 6.5FHD+na kumfanya mtumiaji aweze kuangalia vizuri picha zake vizuri huku ikiwa na sehemu maalum ya kujiremba (Beautify)”.

“Muonekano wa nyuma ina kamera kubwa ya mega pixel 64 ambayo unaweza kupiga picha eneo kubwa zaidi na ina kamera saidizi tatu. “Muonekano wa ndani ina procesa kubwa ya G95 inayomfanya mtumiaji aweze kudownload vitu kiurahisi au kucheza gemu kirahisi.

“Ina betri kubwa sana yenye uwezo wa miliums 5000, ambayo ina uwezo wa kuhifadhi chaji kwa muda mrefu pia ina storage kubwa ya GB 128 Ram 8 na haina shida ya external memory”.

“Infinix Note 10 Pro ina OTG yaani USB Conector ambayo unaweza kuchomeka flash, mouth.

“Sifa yake nyingine ni kuwa na Adroid 11 ambayo ina vitu kibao vitakavyokufanya uifurahie simu yako”.

Join our Newsletter