Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 14Article 563146

LifeStyle of Thursday, 14 October 2021

Chanzo: eatv.tv

Instagram kutoa taarifa kukitokea tatizo la kiufundi

Instagram kutoa taarifa kukitokea tatizo la kiufundi Instagram kutoa taarifa kukitokea tatizo la kiufundi

Kufuatia tatizo la kimtandao ambalo lilitokea siku za hivi karibuni na kuzua taharuki kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, sasa Instagram imeanza majaribio ya programu 'feature' mpya ambayo itakuwa ikitoa taarifa pale linapojitokeza tatizo la kiufundi.

Taarifa hiyo itakuwa ikitokea kwa mfumo wa notification kwenye ukurasa wa mtumiaji wa mtandao huo kumjulisha kuwa limejitokeza tatizo la kiufundi ambapo baada ya mafanikio huduma hiyo itasambaa ulimwenguni kote.