Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 22Article 573349

Burudani of Monday, 22 November 2021

Chanzo: BBC

Justin Bieber aagizwa kufuta tamasha lake Saudi Arabia, sababu hizi hapa

Justin Bieber aagizwa kufuta tamasha lake Saudi Arabia, sababu hizi hapa Justin Bieber aagizwa kufuta tamasha lake Saudi Arabia, sababu hizi hapa

Mchumba wa mwanahabari aliyeuawa Jamal Khashoggi amemtaka Justin Bieber kufuta tamasha lake lijalo nchini Saudi Arabia mwezi ujao.

Mwimbaji huyo wa Canada ni miongoni mwa ‘mastaa’ wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye mashindano ya kwanza ya magari ya Formula One Grand Prix huko Jeddah.

Lakini Hatice Cengiz aliandika barua ya wazi kwa Bieber akimtaka "kutuma ujumbe mzito" kwa kujiondoa.

Khashoggi, mkosoaji mashuhuri wa utawala wa Saudia, aliuawa katika ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul Oktoba 2018, alikoenda kuchukua nyaraka za harusi ya wanandoa hao. Mwili wa mwanahabari huyo uliagwa huku Bi Cengiz akisubiri nje.

"Usiwaimbie wauaji wa mpendwa wangu Jamal," Bi Cengiz aliandika katika barua hiyo iliyochapishwa katika gazeti la Washington Post.

Alisema Bieber alikuwa na "fursa ya kipekee" ya kuonyesha kwamba "jina na kipaji chake havitatumika kurejesha sifa ya utawala unaoua wakosoaji wake".

Bieber anatazamiwa kuteka vyombo vya habari kwenye mbio za F1 tarehe 5 Desemba, akijumuika na wasanii wengine wakiwemo A$AP Rocky, David Guetta na Jason Derulo.