Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 21Article 573187

Burudani of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Jux: Bongo Unafiki Mwingi

Juma Jux Juma Jux

MKALI wa RnB Bongo, Juma Mussa au Jux anafunguka kuwa, wasanii wamekuwa na unafiki mwingi kuliko kufanya kazi.

Jux anatoa ushauri wa wasanii wenzake kwamba, wanahitaji kuwa na mioyo ya kusaidiana wao kwa wao huku akiamini hiyo ndiyo njia mojawapo ya kuupeleka mbali muziki Bongo Fleva.

“Sisi wenyewe inabidi tuwe na moyo wa kusaidiana, unajua kuna sehemu unaona kabisa kwamba inamfaa mtu f’lani, tusisite kupeana sapoti, maana wasanii tumekuwa na unafki mwingi, tunanafikiana sana.

“Hatuwezi kubadilisha, lakini kikubwa tuwe na upendo ili ila isifike wakati tutake kuuana kwa sababu ya vitu ambavyo vinapita tu,” anasema Jux.