Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 07 12Article 546673

Burudani of Monday, 12 July 2021

Chanzo: ippmedia.com

Jux kusaidia muziki wa asili Kahama

Jux kusaidia muziki wa asili Kahama Jux kusaidia muziki wa asili Kahama

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Arbab MB Entertainment and African Boy, Mbwana Imamu wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya ujio wa Jux wilayani hapa katika tamasha linalojulikana kwa jina la ”Jux live in Kahama” na litakalofanyika Julai 30 mwaka huu.

Alisema kuwa, waandaji wengi wa matamasha hivi sasa wamekuwa wakitumia miziki ya kizazi kipya kuwaburudisha wananchi, hali ambayo inafanya miziki ya asili kutokupendwa na wasikilizaji.

“Mimi katika uandaaji wangu wa nyimbo za kizazi kipya sijawahi kuhusika na uandaaji wa ngoma na muziki wa asili, hili nitalichukua na kulifanyia kazi na nitaanza nalo kwa kiasi kikubwa na wasanii wa ngoma za asilia wa Tanga ambako ndiko natokea,” alisema Imamu.

Aliongeza kusema, Jux anampango wa kuibua vipaji vya ngoma za asili zinazopigwa pembezoni mwa vijiji ili na wao waweze kutamba katika matamasha mbalimbali hapa nchini.