Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 08Article 584077

Burudani of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kajala: Nimepisha Mitandao Kwanza

Kajala: Nimepisha Mitandao Kwanza Kajala: Nimepisha Mitandao Kwanza

STAA mwenye shepu yake kunako Bongo Movies, Kajala Masanja anasema kuwa, ameipisha kidogo mitandao ya kijamii ili watu waendelee na shughuli zao maana kila siku akifikiria mambo ya mitandao, yanampotezea muda wake mwingi.

Katika mahojiano Kajala anasema kuwa,kuna wakati mtu anakubali tu kuandamwa na mitandao ya kijamii, akiamini kuna muda watanyamaza na mtu utaendelea na mambo yako vizuri kama ilivyokuwa mimi kwangu huko nyuma nilivyoandamwa na mtoto wangu (Paula).

“Kwa sasa nimeipisha mitandao kwanza iendelee na kazi zake nyingine, maana kila kukicha ilikuwa ni mimi, lakini mwisho wa siku nilikubali tu kila kitu nikaa kimya na mwisho wa siku walitusema na wakamaliza yote, wakatulia tuli,” anasema Kajala.