Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 06Article 541294

Burudani of Sunday, 6 June 2021

Chanzo: eatv.tv

"Kama jela shule, mpeleke Mwanao" - Amber Rutty |

"Kama jela shule, mpeleke Mwanao" - Amber Rutty |

Kuna ile kauli ambayo inasemwa kwamba jela ni sehemu ya mafunzo lakini msanii Amber Rutty ameonekana kuipinga kauli hiyo kwa kusema anayeona jela ni sehemu ya mafunzo basi ampeleke mtoto wake au ndugu yake akajionee.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumapili , 6th Jun , 2021 Msanii Amber Rutty

Amber Rutty amesema hivyo baada ya yeye mume wake Said Bakary kurudi Uraiani ambapo walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa matatu ikiwemo kuvuja kwa video isiyo na maadaili na kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

"Jela ni ngumu na sio nzuri, japo kuna watu utawasikia wanasema jela shule nenda ukajifunze lakini mimi nakataa jela sio shule bali ni ngumu, nimejifunza mengi sana kwa sababu nimeumizwa na mitihani mingi niliyopitia"

"Mtu akisikia umeenda jela anakuona kama una makosa au nuksi, jela ni mbaya na mateso, kama unaona jela shule mpeleke mwanao au ndugu yako" ameongeza Amber Rutty 

Kwa sasa Amber Rutty na mume wake wanatamba na wimbo wao mpya unaoitwa jela ambao unahamisha watu wasifanye vitu sivyo ambavyo vitawapeleka jela.

Join our Newsletter