Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 17Article 543199

Filamu of Thursday, 17 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Kifo cha Kanumba chaweka rekodi

Kifo cha Kanumba chaweka rekodi Kifo cha Kanumba chaweka rekodi

Meneja Mkuu wa magazeti ya Udaku Abdallah Mrisho 'Abby Cool' amesema msanii aliyeweka rekodi katika magazeti pendwa kwenye mauzo ni kifo cha Marehemu Steven Kanumba japo halikuwa tukio zuri.

Submitted by Shaluwa Anta on Alhamisi , 17th Jun , 2021 Steven Kanumba enzi za uhai wake

Akifunguka hilo kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio, Abby Cool amesema kipindi hiko hakukuwa na 'source information' kama magazeti na yalikuwa yananguvu na yanaaminika.

"Sio vizuri kuzungumzia halikuwa tukio zuri lakini msanii ambaye aliweka rekodi katika magazeti pendwa kwenye kuuza ni kifo cha marehemu Steven Kanumba, kipindi hicho hakukuwa na source formation nyingine kama magazeti, yalikuwa yana nguvu, kuaminika na wasanii waliyaamini" 

"Kwa bahati mbaya lilipotokea tukio hilo la msiba watu wengi sana walifuatilia kwenye magazeti mtu alitaka kujua habari, nini kilichotokea mpaka amefariki na maziko yake" ameongeza Abby Cool

Imepita miaka 9 sasa tangu alipofariki staa huyo wa filamu Steven Kanumba mwaka 2012, na alizikwa katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.