Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 24Article 553420

Burudani of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Kinachoendelea kwenye afya ya Jose Chameleon

Kinachoendelea kwenye afya ya Jose Chameleon Kinachoendelea kwenye afya ya Jose Chameleon

Kwa mara ya kwanza baada ya kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi msanii Jose Chameleon amemshukuru mama yake kwa kumpambania na kumuonyesha upendo katika kipindi.

Jose Chameleon ametoa ujumbe huo kwa mama yake kupitia page yake ya Instagram baada ya kushea picha akiwa amelala Hospitalini kwa kuandika maneno yafuatayo.

"Ahsante Mama, upendo wako uko dhahiri, hujawahi kukata tamaa juu ya ukweli, nitakua na nguvu ya kujifunza kutoka kwako. Mungu akujalie uzima zaidi"

Siku ya Jumapili zilitoka taarifa za kulazwa kwa muda wa wiki moja kwa msanii huyo ambaye anasumbuliwa na tatizo la ini na kongosho.