Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 16Article 551734

Burudani of Monday, 16 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kolabo za kimataifa zinazosubiriwa kwa hamu

Diamond Platnumz kwenye Picha akiwa na Wiz Khalifa Diamond Platnumz kwenye Picha akiwa na Wiz Khalifa

Miezi kadhaa iliyopita baadhi ya wasanii wa Bongofleva walionekana wakiwa studio wakirekodi na wasanii tofauti wa kimataifa wenye majina makubwa kutokaa Marekani na Nigeria.

Hatua hiyo imewafanya mashabiki kuwa na hamu ya kusikia muziki utakaozalishwa. Hizi ni miongoni mwa kolabo ambazo zinasubiriwa na mashabiki.

1. Diamond X Wiz Khalifa

Juni, mwaka huu, Diamond Platnumz alikwenda Marekani kwa ajili ya tuzo za BET. Akiwa huko alikutana na wasanii mbalimbali na kuingia nao studio kurekodi nyimbo ambazo zinatarajiwa kuwepo kwenye albamu yake ya nne.

Miongoni mwa wasanii hao ni Rapa Wiz Khalifa aliyetoa wimbo maarufu wa maombolezo uitwao See You Again akishirikiana na Charlie Puth wengine ni Busta Ryhmes, Akon na Snoop Dogg.

2. Hamisa Mobetto X Mr.P (P Square)

Wiki mbili zilizopita Hamisa Mobetto aliendaNigeria na akiwa huko amerekodi wimbo na Mr. P wa kundi la P Square ambaye pia ameshirikishwa na Vanessa Mdee katika wimbo wake uitwao Kisela.

Akiwa huko pia amefanya video ya wimbo aliorekodi toka mwaka jana na Korede Bello na ikumbukwe pia tayari Hamisa alishawahi kutoa wimbo na msanii wa Nigeria, Singah aliyemshirikisha katika ngoma yake ya Ginger Me.

3. Harmonize X Master KG

Master KG alikuja nchini Desemba 2020 kufanya shoo ‘Life is Breeze’ ambayo Harmonize alitokea na kutumbuiza kwa muda mfupi.

Kabla hata ya shoo hiyo wawili hao walionekana studio na kisha Master KG aliongea kwenye moja ya vituo vya redio na kuthibitisha uwepo wa kolabo hiyo. Tayari Harmonize amefanya kazi na wasanii wakubwa Afrika kama Yemi Alade, Emma Nyra, Eddy, Korede Bello, Marina, Sarkodie na kadhalika.

4.Nandy X Yemi Alade

Kolabo ya wawili hawa imekuwa ikizungumzwa kwa muda mrefu huku Nandy akieleza tayari walisharekodi nyimbo mbili kipindi kirefu ila bado wakati wa kuzitoa haujafika.

Nandy na Yemi Alade walikutana 2016 nchini Nigeria katika shindano la kwanza la karaoke barani Afrika, Tecno Own The Stage lilofanyika nchini humo ambapo Nandy alishika nafasi ya pili na kupata Sh36 milioni.

5. Konde Music X Davido

Harmonize na wenzake Ibraah na Country Boy aliowasaini kwenye lebo yake ya Konde Music Worldwide, Aprili, mwaka huu walienda Nigeria na kupokewa na mwenyeji wao, Young Skales ambaye naye akasainiwa na lebo hiyo.

Wakiwa huko walionekana studio na Davido ila bado haijajulikana kolabo na mkali huyo ni ya nani kati yao. Hadi sasa Davido ameshafanya kazi na wasanii wa Tanzania kama Diamond, Joh Makini na Dayna Nyange.