Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 29Article 560335

LifeStyle of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: Bbcswahili

Kutana na mwanamke mwenye hofu ya wanaume

Jacinta Wambui Jacinta Wambui

Hisia zake na mawazo yake pamoja na upeo wake hususani kuhusu jinsia ya kiume au wanaume kwa ujumla, ni tofauti mno na ile ya wanawake wengi wa rika lake .

Mwanadada Jacinta amewekawazi kuwa hali hiyo inammsumbua sana na inawapa wasiwasi watu anaoishi nao kila anapokuwa karibu na wanaume.

Jacinta amekiri kuwa huapatwa na uwoga pale ambapo mwanaume akimkaribia hushindwa kujizuia.Hata hivyo mwanadada huyo anasema hali alionayo ni yakisaikolojia na na pia ni ugonjwa wa akili, nakukiri kuwa ni hali amabyo amepambana nayo tangu akiwa binti mdogo.

"Mara nyingi nawaza nawezaje kuweka bango amabalo litaeleza kuwa mimi siwezi kuongea maaana kila napokwena nasemeshwa na ninabaki kimya". amesema Jacinta

Jacinta amesema mara nyingi inapojitokeza kwenye vyombo vya habari huwa anajipa moyo wakuwa jasiri kuzunguzia hali yake lakini hupata wasiwasi mkubwa kila akiwaza watu wanamchukuliaje .

Jacinta amekiri kuwa anaishi na hali ambayo inajulikanayo kitaalamu 'anthrophobia ' ikitafsiriwa na wataalamu wa magonjwa ya kiakili kama hofu ya watu au kitu kingine chochote .Hali kadhalika Jacinta anakiri kuwa ana changamoto ya kuwa na watu , kama watu wengine kwa mfano yeye huhisi ni vigumu kuanza mawasiliano na watu au kushiriki mazungumzo ya aina yoyote.

Jacinta mwenye umri wa miaka 24 amesema amapaka sasa anashindwa kuelewa namna ya kukabiliana na shida hiyo. anakiri kufwata na wanaume wengi lakini ananjikuta nashinda kuwa kenye mahusiano na haimanishi kuwa havutiwi na jinsia yakiume.

Kwa sasa Jacinta anapata matibabu ya kisaikolojia na mshauri mwanasaikolojia wake ni Bi Mercy Ogonda kutoka nchini Kenya . Kama mwanasaikolojia amethibitisha kuwa Jacinta anaishi na hali ya kuwa na wasiwasi na hofu kuu ambayo kiini chake ni matukio ya kuogopesha yaliofanyika utotoni mwake.

Kulingana na mwanasaikolojia huyu ni kuwa Jacinta na watu kama yeye ambao hupitia mateso ,dhuluma za kimwili au za kingono wakiwa watoto wengi huathirika katika siku za utu uzima wao , hasa iwapo hawatapata fursa ya kujadili yaliowatokea wakiwa wadogo .

Mwanasaikolojia Bi.Mercy Ogonda amesema, Uoga wa watu (Social phobia) ni uoga uliozidi wa watu au hali ya kijamii. Aliyeathiriwa hudhani atatuhumiwa na kupelelezwa na wengine.

Watu walio na uoga wa watu hutatizika na hufanya lolote wawezalo kuepukana na watu au kuwavumilia. Wao huwa hawafanyi mambo ambayo wangefanya kwa kawaida kwa sababu wapo mbele ya watu.

Watajaribu kujizuia kula, kuongea, kuandika au kunywa kwa njia ya kawaida ama kujitenga na watu.

Je, kuna tiba?

Magonjwa ya wasiwasi yanatibika kikamilifu ingawaje kila ugonjwa au aina ya ugonjwa wa wasiwasi una dalili zake. Magonjwa mengi hutibika kupitia matibabu ya kisaikolojia au dawa.

Matibabu yanayotumia mbinu za kisaikolojia pamoja na dawa huwa na matokeo bora yanayodumu. Matibabu kamili ya anxiety disorder ni kama;

• Mbinu za kisaikolojia kama urekebishaji wa tabia (Cognitive Behavioural Therapy CBT) zinazolenga kubadilisha mawazo, tabia na imani zinazoleta wasiwasi. Mbinu hizi zaweza pia kumfanya aliyeathiriwa kupitia yale mambo yanayosababisha wasiwasi (yaani desensitization).

• Mbinu za kupunguza wasiwasi na kutulia.

• Dawa zinazopunguza huzuni ni muhimu katika kutibu wasiwasi fulani na pia kutibu huzuni.

• Dawa ya wasiwasi inayolenga akili pia ni muhimu

• Madawa hayatatibu wasiwasi lakini hupunguza dalili za ugonjwa huu mtu apatapo matibabu ya kisaikolojia. Jamii na marafiki wa watu walio na wasiwasi mara nyingi hutatizika. Usaidizi na elimu ni muhimu kwa kutibu ugonjwa huoJacinta Wambui