Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 06Article 555511

Burudani of Monday, 6 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Lawama za Kala Jeremiah kwa wazee wenye pesa

Lawama za Kala Jeremiah kwa wazee wenye pesa Lawama za Kala Jeremiah kwa wazee wenye pesa

Msanii Kala Jeremiah amesema watu wenye pesa wanaongoza kuharibu mahusiano ya watu kwa sababu changamoto nyingi kwenye jamii inaanzia kwenye ishu za kimahusiano.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumatatu , 6th Sep , 2021 Picha ya msanii Kala Jeremiah

Kala anasema wazee wenye pesa wanapokonya wake na wapenzi wa watu, husababisha maumivu, kilio pia husababisha hata mtu kuongea peke yake ambapo ukichunguza chanzo ni mahusiano.

"Watu wenye pesa wanapokonya wake na wapenzi wa watu na hicho ni kitu kibaya na imekuwa kilio na maumivu mengi"

"Changamoto kubwa ya jamii kwa sasa inaanzia kwenye mahusiano, ukikuta mtu kavurugwa anaongea peke yake ukichunguza chanzo chake nyuma ni mahusiano ndio yamesababisha"

Kala Jeremiah ameongeza kusema watu wenye pesa hawaharibu mahusiano au ndoa za watu pkee bali wanaharibu mpaka future za watu.