Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 24Article 573871

Burudani of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Lynn: Fahyma, Rayvanny Hawajaachana

Lynn: Fahyma, Rayvanny Hawajaachana Lynn: Fahyma, Rayvanny Hawajaachana

VIDEO vixen na msanii wa Bongo Fleva, Official Lyyn ni rafiki au shogale mkubwa wa baby mama wa Rayvanny, Fahyma ambaye ametoboa siri nzito juu ya penzi la wawili hao.

Lyyn ambaye muda mwingi anakuwa na Fahyma anasema kuwa, anachojua ni kwamba Rayvanny na Fahyma hawajaachana kama wengio wanavyoamini.

Inafahamika kwamba, Rayvanny kwa sasa penzi lake na mrembo Paula Kajala limetaradadi.

Anasema wawili hao wapo pamoja na wataendelea kuwa hivyo kwa hiyo wanaoamini wameachana, basi wakae kwa kutulia.

Fahyma anasema ili kuthibitisha hilo ni kitendo cha Rayvanny kumposti mwanamama huyo kwenye Insta Story kabla ya upepo kuchafuka na kumuondoa.

“Mbona Fahyma na Rayvany wapo pamoja? Unataka kuniambia Rayvanny alikosea kumposti Fahyma? Hivi mimi leo ninaweza kukosea nikamposti Diamond?

Inawezekanaje ukawa umeachana na mtu halafu ukakosea ukamposti kwenye Instagram? Unakoseaje?

“Ninavyojua mimi Rayvanny na Fahyma hawajaacha wapo wote na hawataachana. Hata asubuhi nimeongea na Fahyma hana tatizo na Rayvanny…”

“Kuhusu penzi la Rayvanny na Paula sijawahi kulifuatilia. Ninachojua Fahyma ana amani na furaha,” anasema Lyyn ambaye aliwahi kukiri kuwa mpenzi wa Diamond wa zamani.